HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 6, 2024

RAIS MWINYI AKUTANA NA KAMPUNI ZA UWEKEZAJI CHINA

 





RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameendelea na ziara yake jijini Shanghai, China. Leo na kukutana na ujumbe ulioongozwa na Bw. Bai Yin Zhan kutoka kampuni ya China Harbour Engineering Co. Ltd, waliofika katika jengo la Ling Hang Group.

Kampuni hiyo, ina uzoefu wa kujenga miradi ya kimkakati kama vile ujenzi wa bandari, upanuzi, na uboreshaji wa miundombinu kwa viwango vya kimataifa.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo katika 
mchakato wa kuipa dhamana kampuni hiyo
ya China Harbour Engineering Co. Ltd kujenga Bandari ya Mangapwani, Unguja. 

Katika mkutano huo, Rais Dk. Mwinyi amemhakikishia Bw. Bai Yin Zhan kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, baada ya kukamilisha mchakato wa maridhiano kwa pande zote mbili, SMZ itatoa ushirikiano ili ujenzi wa mradi huo uanze mara moja.

Wakati huo huo, Rais Dk. Mwinyi amekutana na wawakilishi wa kampuni mbalimbali ambazo zimeonesha nia ya kuwekeza Zanzibar, zikiwemo Fuhai Group, inayojihusisha na masuala ya nishati, mafuta, na gesi; Chery Holding Group Co. Ltd, iliyobobea katika utengenezaji wa magari yanayotumia nishati ya umeme; na China Sinopharm International, kampuni kubwa inayotengeneza madawa ya binadamu. Mazungumzo hayo yalilenga kuweka misingi ya ushirikiano itakayosaidia kukuza uchumi na kuboresha huduma muhimu kwa wananchi kupitia uwekezaji endelevu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad