HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 9, 2024

KARIMJEE GROUP YAZINDUA KITUO CHA KUTOA HUDUMA ZA MAGARI NCHINI

 Mkurugenzi wa Kitaifa wa Karimjee Group, Amit Singh akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha kisasa cha huduma za magari, Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam Novemba 08, 2024 jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Masoko wa Karimjee Group, Cobus Van Zyl  akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha kisasa cha huduma za magari, Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam Novemba 08, 2024 jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Toyota Tsusho Corporation, Hiroshi Harusawa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha kisasa cha huduma za magari, uzinduzi uliofanyika Novemba 08, 2024 jijini Dar es Saalaam.
Meneja Huduma, Manoj Vishani akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kituo cha kisasa cha huduma za magari, uzinduzi uliofanyika Novemba 08, 2024 jijini Dar es Saalaam.

KATIKA kuleta mapinduzi katika sekta ya huduma za magari, Karimjee Group imeendelea kutoa elimu na kuuza vifaa vya magari vinavyoweza kuzuia ajari za barabarani. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha kisasa cha kutoa huduma za magari nchini jijini Dar es Salaam leo Novemba 8, 2024,  Mkurugenzi wa Kitaifa wa Karimjee Group, Amit Singh amesema uzinduzi huo ni sehemu ya  kujali huduma bora za magari ili kuendelea kuwa salama.

Amesema kituo hicho hakitakuwa cha kawaida bali kitakuwa ni kituo ambacho kimesheheni huduma na maduka ya rejareja, yanayokidhi mahitaji yote ya magari chini.

Pia kitakuwa pia Kituo cha Huduma za Magari kinachohakikisha kuwa wateja wanaweza kuamini kuwa magari yao yako mikono salama.

"Tunafurahi kufungua Kituo cha huduma za Magari kwa umma, tunaamini kuwa mradi huu utaweka kiwango kipya cha huduma za magari nchini Tanzania." Amesema

Kwa Upande wa Afisa Mkuu wa Masoko wa Karimjee Group, Cobus Van Zyl amesema kiituo cha Huduma za Magari kinatoa huduma mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa kina wenye kutumia mitambo ya kisasa, matengenezo makubwa na madogo ya magari, ukaguzi na uingizaji wa betri, huduma za matairi, kuunganisha magurudumu, uratibu wa magurudumu, huduma ya kurekebisha kiyoyozi, na uingizaji wa vipuri kama vile breki. 

Pia amesema kuwa Kituo hicho kinatoa promosheni mbili maalum kwa Wateja wanaweza kupata huduma ya kubadilisha mafuta ya injini kuanzia TSh 50,000 (ikiwemo VAT), ambayo inajumuisha mafuta ya injini, uingizaji wa kichujio cha mafuta na gharama za kazi. 

Aidha kwa wateja wanaonunua matairi 4 ya Goodyear, Otani, au Armstrong watapata huduma ya kuunganisha magurudumu, uratibu wa magurudumu, na kujazwa hewa ya nitrojeni bure.

 "Tunapoendelea kukua na miradi mipya, tunabaki na dhamira yetu ya kutoa huduma bora kwa wateja wetu. Kituo cha Huduma za Magari kinaakisi maono yetu ya kuweka kiwango kipya cha huduma za magari nchini Tanzania."

Pia Karimjee Group imewakaribisha wateja na wadau wote kufurahia huduma za Kituo cha Huduma za Magari.

"Tunaamini kuwa njia bora ya kuelewa ubora tunaotoa ni kuupitia na kupata huduma zetu." Amewakaribisha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad