HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 20, 2024

DKT. MWIGULU MGENI RASMI CHUO CHA KODI

MKuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Profesa Isaya Jairo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 20, 2024 wakati wa kutangaza siku ya Mahafali ya chuo cha Kodi yatakayofanyika Novemba 22, 2024.

WAHITIMU 417 wanatarajia kutunukiwa vyeti katika Mahafali ya 17 ya Chuo cha Kodi (ITA) na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika mahafali hayo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Novemba 20, Mkuu wa Chuo cha ITA, Prof. Isaya Jairo amesema mgeni rasmi huyo atawatunuku vyeti wanafunzi hao wa Stashahada,Shahada na Stashahada ya Uzamilikwa wahitimu hao  wa mwaka wa masomo 2023/2024.

Amesema wahitimu 236 ni wa kiume na wahitimu 181 ni wa kike ambapo wahitimu 195 watatunukiwa cheti cha Uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki yaani the East African Customs and Freight Fowarding Practising Certificate (EACFFPC).

Amesema pia wahitimu 28 watatunukiwa Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani Basic Technician Certificate in Customs and Tax Management (CCTM) huku wahitimu 61 watatunukiwa Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani Diploma in Customs and Tax Management(DCTM).

''Wahitimu 119 watatunukiwa Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi yaaniBachelor Degree of Customs and Tax Management (BCTM)na Wahitimu 14 watatunukiwa Stashahada ya Uzamili katikaKodi yaani Postgraduate Diploma in Tanzania,''alisema.

Jairo amesema mahafali hayo yanafanyika wakati chuo hicho kinajivunia mafanikio mengi katika utekelezaji wa mpango mkakati wa tano wa Chuo ambao umejikita katika kutoa mafunzo kwa njia ya kisasa za kidigitali.

''Tayari maandalizi ya kutoa elimu masafa kwa njia ya mtandao yameanza na yanaendelea vizuri ambapo tunatarajia mafunzo ya elimu masafa yatakapoanza yataongeza idadi ya wanafunzi wanaopata mafunzo katika chuo pamoja na kufikia wanafunzi wengi kwa njia rahisi na kwa wakati mmoja na gharama nafuu na kuongeza idadi ya wahitimu,''alisema.

Amesema kufanyika kwa mahafali ni fursa ya kuwapongeza wahitimu pamoja na kutathminimafanikio na shughuli ambazo zinafanywa na Chuo .

Jairo amesema Chuo hicho mahsusi kwaajili ya kutoa mafunzo ya Forodha na Kodi katika ngazi ya Astashahada,Stashahada,Shahada na Shahada ya Uzamili ambapo kinatoa mafunzo yanayoendana na mabadiliko ya sayansi ,teknolojia na uchumi ambayo yanakidhi mahitaji ya soko la wataalamu wanaohitaji katika nyanja ya forodha na kodi hapa nchini,barani Afrika na Ulimwwenguni.

Aidha amesema kuwa pamoja na jukumu kubwa la kutoa mafunzo kwa watumishi wa TRA,Chuo cha Kodi pia kinatoa mafunzo na ushauri elekezi kwa wadau wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mamlaka nyingine za Mapato Afrika ikiwemo Zanzibar, Sudan, Botswan na Somalia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad