POLISI Kata ya Ikoma Tarafa ya Grumet Wilayani Serengeti mkoani Mara CPL Emmanuel Mwikwabe amekabidhi kiti mwendo kwa mtoto Vaileth Enock(16) mwenye ulemavu wa kuzaliwa ambapo umesababisha kupooza.
Akizungumza wakati akikabidhi kiti mwendo hicho ,CPL Mwikwabe amesema alimbaini Mtoto huyo kupitia kampeni ya utoaji wa elimu ya Polisi Jamii Elimu Nyumba kwa Nyumba katika Kijiji cha Parknyigoti katika kitongoji cha Park B kupitia baba yake mzazi Mzee Enonck Komanya.
"Nilifanikiwa kufika nyumbani kwa Mzee Enonck Komanya nakuwakuta watoto wake na miongoni mwa watoto niliowakuta kwenye mji huo ni pamoja na binti huyu Vaileth , hivyo nikaamua nimshirikishe Mkuu wa Wilaya Bi.kemirembe na kukubali kunishika mkono kwa kunipa kiti mwendo,amesema CPL Emanuel Mwikwabe.
Pia amesema amekabidhi kiti hicho kwa lengo la kupeleka faraja kwa mtoto huyo ambaye toka azaliwe amekuwa akiishi kwa kulala kutokana na kukosa kiti mwendo.
Ametumia nafasi hiyo kuwa kuwataka Wazazi pamoja na wakazi katika kata hiyo kuacha kuwabagua watoto wenye ulemavu waliopo kwenye maeneo yao kwani kufanya hivyo nikuwafanyia ukatili
Jamani poleni asee
ReplyDelete