Na Mwandishi wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi amesema ujenzi unaoendelea wa tanki kubwa la kuhifadhia maji safi kutoka Ruvu unatarajia kukamilika mapema mwakani ambapo litasaidia kuondoa kero ya maji Jijini Dar es salaam.
Waziri ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi na kuzungumza na wananchi wa Banguko katika Jimbo la Ukonga jijini Dar es salaam leo Oktoba 09, 2024.
Ameeleza ujenzi wa bwawa hilo utanufaisha wananchi takribani 450000 hasa wa Jimbo la Ukonga na Segerea na Mkandarasi ameshalipwa fedha zote hivyo mradi utakapokamilika wananchi wote wataunganishwa na mtandao wa maji.
“Hivyo tutashuhudia kata saba katika Jimbo la Ukonga zitakazoondokana na adhaa ya upatikanaji wa maji,” alisema Waziri Lukuvi.
Aidha tunashuhudia fedha nyingi zinatolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji na barabara na tumekubaliana usanishaji wa mikataba ufanyike katika maeneo husika ya ujenzi wa miradi.
Ujenzi wa Miradi ya Maendeleo ni hatua lakini sisi tumekwenda kasi sana katika utekelezaji wake hivyo wananchi mukiona vinaelea vimeundwa,
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe, Albert Chalamila amesema Mkoa umejikita sana katika kulinda amani na kuendelea kulinda raia na mali zao, ili wananchi waweze kujikita katika shughuli za uzalishaji.
“Mwenyeviti wa Serikali za Mitaa na kamati za ulinzi kwa kushirikisha na polisi jamiii, hakikisheni Madhila ya wananchi kuogopa wahalifu yanadhibitiwa katika maeneo yenu,“ alisema Mkuu wa Mkoa Chalamila.
Awali Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amesema Serikali imejenga madarasa ya ghorofa zaidi ya 80 na madarasa ya kawaida 465 kwa shule za sekondari, na kwa upande wa shule za msingi madarasa zaidi ya 437 yamejengwa.
“Mafanikio haya yanakuja kutokana na mahusiano tuliyonayao na wawakiishi wa wananchi wanaochagiza kwa kiasi kikubwa maendeleo ya miradi ya maendeleo,” alisema Mkuu wa wilaya Mpogolo.
“Mradi wa Tanki la Maji Bangulo mbioni kukamilika” Waziri Lukuvi Na Mwandishi wetu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi amesema ujenzi unaoendelea wa tanki kubwa la kuhifadhia maji safi kutoka Ruvu unatarajia kukamilika mapema mwakani ambapo litasaidia kuondoa kero ya maji Jijini Dar es salaam. Waziri ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi na kuzungumza na wananchi wa Banguko katika Jimbo la Ukonga jijini Dar es salaam leo tarehe 09/10/2024.
Ameeleza ujenzi wa bwawa hilo utanufaisha wananchi takribani 450000 hasa wa Jimbo la Ukonga na Segerea na Mkandarasi ameshalipwa fedha zote hivyo mradi utakapokamilika wananchi wote wataunganishwa na mtandao wa maji. “Hivyo tutashuhudia kata saba katika Jimbo la Ukonga zitakazoondokana na adhaa ya upatikanaji wa maji,” alisema Waziri Lukuvi. Aidha tunashuhudia fedha nyingi zinatolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji na barabara.
Ikumbukwe katika ziara hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe William Lukuvi, alizindua Mradi wa Barabara ya Tukuyu Ilala na Kuweka Jiwe la Msingi katika sekondari Liwiti.
Licha ya hayo pia Lukuvi amesema kuwa mwezi huu kuanzia oktoba 11 mpaka 27, kutakuwa na kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi wa Serikali ya mtaa utakaofanyika Novemba 27,2024 Tanzania nzima. ili Kkumchagua kiongozi unayemtaka.
"Na ili uwe na haki lazima ajiandikishe ili kutumia haki yako kuchagua kiongozi unayemtaka..... Na umchague kiongozi aliyekuwa nawe kwenye shida na raha" Amesema Lukuvi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe William Lukuvi akiwa pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azan Zungu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila wakati wa uzinduzi wa Barabara ya Tukuyu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe William Lukuvi akikagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi Tanki la Maji liliopo Pugu Stesheni Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe William Lukuvi akikagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi Tanki la Maji Bangulo liliopo Pugu Stesheni Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe William Lukuvi akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila akiweka jiwe la Msingi katika shule ya sekondari Liwiti iliyopo Segerea Jijini Dar es Salam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe William Lukuvi akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Robert Chalamila wakipata maelezo yamchoro wa mradi wa ujenzi wa tanki la maji Banguko lililoo Pugu Stesheni Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Bangulo mara baaada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa tanki la Maji lililopo Pugu Station.
No comments:
Post a Comment