Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Profesa Othman Chande Othman amesema Tanzania ipo vizuri kwenye masuala ya viwango ambapo inajitaidi kuandaa viwango katika kila sekta ambazo zinasaidia katika uchumi na biashara ili viwanda viweze kuzalisha bidhaa zenye viwango
Profesa Othman Chande alitoa kauli hiyo leo Oktoba 30,2024 jijini Dar es Salaam kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani ambapo kwa Tanzania iliadhimishwa mapema Leo
Alisema TBS Inafanya hivyo ili kuwawezesha Watanzania kuuza bidhaa zao nje ya nchi japo tumezoea kuona nchi za nje zinaleta bidhaa zao nchini, lakini na Tanzania inataka iwapelekee pia bidhaa ambazo zinazalishwa na Tanzania na zenye Viwango nje ya nchi.
"Unajua kuna bidhaa nyingi za kwetu ni za asili kama vile asali ambavyo watu wa nje wanavipenda na sisi tunataka tuvizalishe kwa viwango," alisema.
Alitoa raia kwa wafanyabiashara pamoja na wazalishaji wa bidhaa za viwandani na nyingine kuhakikisha bidhaa zinapimwa au kuthibitishwa na TBS kwa kuwa maabara zote za shirika hilo zimepata ithibati, hivyo zikishapimwa na maabara hizo zinaweza kupelekwa duniani kote bila vikwazo vyovyote.
""Tunatoa rai kwa wazalishaji wahakikishe bidhaa wanazozalisha tuzipime ili waweze kuvuka mipaka waweze kuuza nje. Lakini watu wanapenda kupeleka bidhaa zao nje bila kupitia kwetu, wakipeleka tu wakikwama wasilalamike kwa sababu hawajapita kwa mdhibiti wa mambo ya viwango," alisema Profesa Chande Othman.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, David Ndibalema, alisema Leo walikuwa wanaadhimisha Siku ya Viwango Duniani hasa kwa kutambua kwamba TBS jukumu lake kuu ni kuandaa viwango vya kitaifa.
Alisema wanapoandaa viwango vya kitaifa, pia wanashiriki katika ngazi za kimataifa kwa sababu ya utandawazi na muingiliano wa sasa hivi wa teknolojia, hivyo ni lazima watumie viwango ambavyo vinafanana ili kuweza kurahisisha biashara.
"Kwa hiyo Tanzania kupitia TBS ni mwanachama wa Shirika la Viwango Duniani (ISO) hivyo tunaungana na jumuiya ya kimataifa kusherehekea siku hiyo na lengo kuu ni kutambua juhudi na michango wa wataalam mbalimbali ambao wanaandaa viwango vya kimataifa," alisema Ndibalema na kuongeza kuwa wao kama TBS wameendelea kushiriki katika kamati mbalimbali za kuandaa viwango kama wanachama wa ISO .
Pia alisema katika kuadhimisha siku hiyo watakuwa na mafunzo hasa kuhamasisha wadau na wataalam licha ya kushiriki kuandaa viwango, lakini waweze kuwa na mbinu za uongozi waweze kushawishi zaidi kwenye uandaaji wa viwango vya kimataifa.
Alisema viwango vina umuhimu sana katika kuzalisha bidhaa ambazo ni bora na ambazo ni shindani duniani hivyo ni muhimu sana wazalishaji wanaolenga zaidi masoko ya nje kuzingatia viwango ambazo zitatambulika kwenye soko la kimataifa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Profesa Othman Chande Othman akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani ambapo kwa Tanzania iliadhimishwa mapema leo Oktoba 30, 2024.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Profesa Othman Chande Othman akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani ambapo kwa Tanzania iliadhimishwa mapema leo Oktoba 30, 2024
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Profesa Othman Chande Othman akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani ambapo kwa Tanzania iliadhimishwa mapema leo Oktoba 30, 2024
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, David Ndibalema akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani ambapo kwa Tanzania iliadhimishwa mapema leo Oktoba 30, 2024
No comments:
Post a Comment