NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
BENKI
ya NMB na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wamesaini mkataba wa
makubaliano ya ushirikiano, unaolenga Kukuza Vipaji, Ubunifu, Uwekezaji
katika Mageuzi ya Kidigitali na Msaada wa Kifedha kwa wanafunzi wa Chuo
cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Co-ICT), kilicho chini ya chuo
hicho.
Makubaliano
hayo ya miaka mitano, yamesainiwa leo Jumatano Oktoba 23 Makao Makuu ya
NMB jijini Dar es Salaam, UDSM ikiwakilishwa na Naibu Makamu Mkuu wa
Chuo anayeshughulikia Utafiti Profesa Nelson Boniface na NMB
imewakilishwa Afisa Mkuu wa Rasirimali Watu, Emmanuel Akonaay
Akizungumza
kabla ya kusaini mkataba huo, Akonaay alisema NMB ambayo elimu ni sekta
ya kipaumbele, inaamini kuwa makubaliano hayo yanaenda kuchochea
ubunifu miongoni mwa wanafunzi wa Co-ICT, ambao utawezesha utatuzi wa
changamoto mbalimbali zinazoizunguka jamii na taifa kwa ujumla.
Alibainisha
ya kwamba makubaliano hayo yatajikita katika maeneo matano ya; Ukuzaji
Vipaji na Ujuzi, Ukuzaji Ubunifu wa Matumizi ya Teknolojia, Uwekezaji
katika Mageuzi ya Kidigitali, Utafiti Teknolojia na Maarifa, pamoja na
Msaada wa Kifedha wa Masomo kusaidia programu bunifu.
“Katika
Ukuzaji wa Vipaji na Ujuzi, kwa pamoja NMB na Co-ICT tutashirikiana
katika kutambua na kuendeleza kupitia mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi
waliofanya vizuri katika Nyanja za TEHAMA, kama itakavyokuwa kwenye
Ukuzaji wa Ubunifu wa Matumizi ya Teknolojia.
“Hapo
tutasaidia kuendeleza ushindani katika Sekta ya Fedha ambayo inakua kwa
kasi sana, pande zote zitashirikiana katika kutoa fursa kwa wanafunzi
kujaribu teknolojia tofauti zinazoweza kuwa na athari chanya kwa sekta
ya kifedha kupitia SANDBOX,” alifafanua Akonaay.
Aliongeza
ya kwamba, katika Mageuzi ya Kidigitali, NMB na Co-ICT kwa pamoja
watawekeza kwenye nyanja hiyo ili kuongeza ufanisi, kupunguza gharama na
kuboresha huduma kwa wateja na katika Utafiti wa Teknolojia na Maarifa,
watashirikiana kufanya utafiti wa kiteknolojia ili kuchunguza athari
zake kwa Sekta ya Fedha.
“NMB
tunaamini makubaliano haya sio tu yatasiadia kuimarisha mahusiano yetu,
bali ni muendelezo wa mashirikiano endelevu baina yetu na ahadi yetu ni
kuwa NMB itaendelea kufanya kazi na Serikali yetu katika Sekta ya
Elimu, ambayo ni utekelezaji wa dhati wa dhamira yetu ya kuchangia
ukuaji na ustawi wa elimu nchini.
“Tunaishukuru
UDSM Co-ICT kwa kuichagua NMB na kukubaliana kushirikiana katika
kufanikisha matakwa ya kimkataba,” alisema Akonaay aliyemwakilisha Afisa
Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna ambaye alishindwa kuhudhuria
hafla hiyo kutokana na mkwamo wa kimajukumu.
Ukiondoa
makubaliano hayo, mchango na mashirikiano mengine baina ya NMB na UDSM
ni mkataba wa miaka miwili na Shule Kuu ya Biashara ya UDSM, ambako kwa
miaka miwili hii imetumia Sh. Mil. 35 kwa ajili ya kuwazawadia wanafunzi
watatu bora waliofanya vizuri zaidi katika Masomo ya Biashara.
“Pia,
NMB tumekuwa tukiandaa Career Fairs, ambayo tumeyatumia kuwakutanisha
mamia ya wanafunzi, sio tu kuwaonesha aina ya huduma zetu, bali
kuwafunza namna ya kuomba kazi na kuwajengea uelewa wanafunzi
wanaojiandaa kuingia katika soko la ajira, kuwajuza changamoto na
mahitaji ya soko.
“Lakini
pia, kupitia NMB Foundation, tumekuwa tukitoa ufadhili wa NMB Nuru
Yangu Scholarship and Mentorship, ambapo hadi sasa tua wanafunzi 132
wako katika vyuo mbalimbali vya umma, ambako wametengewa kiasi cha Sh.
Bilioni 1.4 ili kuwawezesha kupata masomo yao hasa watokao mazingira
magumu,” alisema.
Aidha,
Akonaay alisema benki yake imekuwa pia ikitoa programu ya mafunzo kwa
vitendo kwa wanafunzi, ambapo jumla ya wanafunzi 1,500 waliomaliza vyuo
vikuu wamekuwa wakifanya mafunzo hayo, wengi wao wakiwa wamechukuliwa na
NMB na wengine wameajiriwa kwingineko
Kwa
upande wake, Profesa Nelson aliishukuru NMB kwa kukubali kuingia
mkataba wa makubaliano hayo, yanayompa uhakika kwamba yanaenda
kuwawezesha vijana wazuri wa ubunifu ambao watanufaika vya kutosha
kupitia makubaliano hayo, yanayoenda pia kuchachua teknolojia ya Akili
Mnembaa ‘Artificial Intelgency’ (AI).
“Tulikupokuwa
tunateta kwamba, AI itakuwa ni sehemu ya mambo ambayo yatatekelezwa
kupitia makubaliano haya, lakini je AI tulizonazo zinajua kuongea lugha
zetu tunapofanya biashara? Sasa hiyo ni ‘challenge’ ambayo tunapaswa
‘kui-address’ kwenye muundo wa kibiashara uliomo kwenye mkataba huu.
“Hii
maana yake ni kuwa itatulazimu tutapowaendea watu wasiojua Kiingereza,
wasiojua Kiswahili, tuweze kuwafikia kwa lugha zao za asili ili
kufanikisha malengo na mipango ya kibiashara. Nadhani hapo NMB itakuwa
‘giants’ wa ubunifu,” alisema Profesa Nelson.
Alibainisha
na kusisitiza kuwa UDSM na Co-ICT inao vijana wengi, wazuri na mahiri
katika katika ubunifu, anaodhani wakati wao kunufaika na makubaliano
hayo ni sasa na kuwataka NMB kusapoti harakati zao sio tui li
kuwawezesha kuingia katika soko la ajira, bali kujiajiri
itakapolazimika.
“Tunawashukuru
sana NMB kwa namna wanavyoyafanyia kazi makubaliano tunayoingia baina
yetu, kwa sababu hii sio mara ya kwanza kusaini mikataba ya aina hii,
kama ilivyotanguliwa kusemwa na Bwana Akonaay, ambako wametupa
uwezeshaji katika Career Fairs na Motisha kwa Shule Kuu ya Biashara,”
alisema Prof. Nelson.
No comments:
Post a Comment