Katika
kuadhimisha siku ya mtoto wa Kike Duniani, Jukwaa la Wanawake katika
Usafiri wa Anga Tanzania (WIA-TZ) kwa kushirikiana na Jukwaa la Viongozi
katika usafiri wa Anga Afrika (Afican Leaders in Aviation-ALA)
wametembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Rolina kilichopo Kwa
Sadala mkoani Kilimanjaro na kutoa elimu na uelewa wa sekta ya Usafiri
wa Anga.
Akizungumza
katika ziara hiyo, Khodana Davhana Mwanzilishi mwenza wa Jukwaa la
Viongozi katika Usafiri wa Anga barani Afrika, ameeleza kuwa
wanatembelea nchi mbalimbali barani Afrika hususani katika shule na
vituo kwa lengo la kuhamasisha vijana hasa wa kike kujiunga na sekta ya
usafiri wa anga.
Amesisitiza
kuwa masomo yoyote ikiwemo sheria, biashara, udaktari, sayansi n.k
yatamuwezesha kijana wa kike kujiunga na sekta ya anga.
Wanachama
wa WAI – TZ Bi Upendo Mwaibale Afisa mtoa taarifa za anga na Bi Fatma
Kawale, Afisa Uongozaji Ndege walitoa elimu ya usafiri wa Anga na
kuwahimiza vijana hasa watoto wa kike kuchukua masomo ya Sayansi,
Teknolojia, Hesabu na Uhandisi ili waweze kuingia katika sekta ya
Usafiri wa anga, lakini pia waliwahimiza kuishi ndoto zao ili kufikia
malengo yao.
Zawadi
mbalimbali zimetolewa na Jukwaa kwa vijana ikiwemo vitabu ili
kuwajengea uelewa mpana zaidi kuhusiana na sekta ya usafiri wa anga na
fursa zilizopo katika sekta.
No comments:
Post a Comment