Mkurugenzi Mtendaji wa DHL Tanzania, Humphrey Pule (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Mtandao wa Vituko Vya Mafuta TotalEnergies, Abdul Rahim Siddique wakati kampuni hizo zolipozindua rasmi ushirikiano wa kibiashara Jijini Dar es Salaam Ijumaa.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya DHL Express kwa kishirikiana na TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, zimezindua ubia wa huduma zao, katika jitihada za kurahisishia zaidi wateja kupata huduma za haraka za kimataifa.
Mteja anayetaka kutuma hati au vifurushi ng'ambo anaweza kwenda kwenye kituo cha huduma cha TotalEnergies kinachotoa huduma za DHL Express ili kusafirisha mizigo yake, kuhakikisha urahisishaji na ufikiaji wa mtandao wa kimataifa wenye nguvu ambao uko chini ya DHL. Hii inajumuisha usafirishaji wote wa ndani na wa kimataifa kwa vituo vikuu katika zaidi ya nchi na maeneo 220 duniani kote.
Wateja wataweza pia kunufaika na bidhaa ya DHL, Express Easy, kwenye vituo vya huduma vya TotalEnergies, ambapo bidhaa ya Express Easy hurahisisha kutuma hati au vifurushi. Wateja wanaweza kuchagua bahasha au mojawapo ya maboksi saba na kulipa bei iliyowekwa kwa ukubwa wa boksi mteja alilochagua, badala ya kulipa ada kulingana na uzito wa kifurushi. Zaidi ya hayo, wateja wataweza kuchagua boksi lao, lipa kiwango kilichowekwa na kutuma hati au kifurushi chao kwa maeneo yoyote ya kimataifa ya DHL.
Mkurugenzi Mtendaji wa DHL Express nchini Tanzania, Humphrey Pule, akikaribisha ubia huu, alisema ubia wao utawanufaisha sana watumiaji nchini kote.
"Sekta ya usafirishaji wa haraka, na hasa huduma za rejareja kwa watumiaji na biashara ndogo ndogo na za kati, zinakuwa muhimu sana barani Afrika. Ili sisi kuhudumia soko hili vizuri zaidi na kufungua fursa za kimataifa kwa wanafunzi, wamiliki wa biashara ndogo ndogo na watumiaji wa jumla, tulihitaji kuongeza ufikiaji wa bidhaa zetu za haraka lakini, wakati huo huo, iwe rahisi na kwa bei nafuu kuzitumia. Kwa hiyo, TotalEnergies ni mbia wa wazi kwetu - si tu kwamba wana biashara thabiti Afrika, bali pia wana mtandao mpana wa rejareja katika bara zima wakiwa na mtandao unaoongoza wa vituo nchini Tanzania ambao unaweza kunufaisha wateja wetu."
“Kama kampuni inayoongoza ya mafuta yenye mtandao mpana wa vituo nchini Tanzania, tunatafuta mara kwa mara njia za kutimiza ahadi ya chapa yetu ya kufanya vituo vya huduma vya TotalEnergies kuwa kituo kimoja ambapo wateja wanaweza kupata huduma zao zote muhimu na leo wateja wanaweza kusafirisha vifurushi vyao duniani kote kupitia DHL wakiwa kwenye vituo vya huduma vya TotalEnergies. Zaidi ya hapo, huu ni mwanzo tu, kwani hiki ni kimojawapo cha vituo vingi vya TotalEnergies ambavyo vitakuwa vikitoa huduma za DHL nchini kote,” alisema Abdul-Rahim Siddique, Mkurugenzi wa Mtandao wa vituko vya mafuta TotalEnergies Tanzania kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu.
No comments:
Post a Comment