SINGIDA
KIONGOZI wa Makundi Muhimu TK Movement Mkoa wa Singida,Ndg Ahmed Misanga (alivaa kofia) amewataka vijana kutumia fursa ya kujiandikisha katika Daftari la Mpiga kura wa Serikali za mitaa ili kutoa fursa ya Kuchagua viongozi wanaowahitaji.Misanga ameyasema hayo wakati alipokutana na vijana Mkoa wa Singida ikiwa ni kuwahamasisha vijana kujiandikisha kutimiza haki ya kupiga kura.
Amesema kuwa vijana kunahitaji kujitambua katika kufanya maamuzi chanya kwenye kuyaendea ikiwemo ya kujiandikisha ili kuchagua wa viongozi wa Vijiji,Vitongoji na Mitaa.
Hata hivyo amesema serikali imeweka mazingira rafiki ya kujiandikisha na kuachana visingizio vya kutojiandikisha.
KIONGOZI wa Makundi Muhimu TK Movement Mkoa wa Singida,Ndg Ahmed Misanga (alivaa kofia) akiendela na uhamasishaji kwa vijana wa mkoa huo kama anavyoonekana katika picha.
No comments:
Post a Comment