HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 10, 2024

Timu ya Umoja Forest yaibuka mshindi katika mashindano ya Bushiri Rede Super Cup

 

Na Mwandishi Wetu


Timu ya Umoja Forest imechukua ubingwa kwa kuibamiza timu ya washngton DC magori Saba dhidi ya Gori moja katika mashindano ya kombe la Bushir Rede Super Cup.

Mashindano hayo yaliyoratibiwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbopo Kata ya Mabwepande Bushir Mziwanda kwa ajili ya kuwajenga vijana katika mazoezi kuepukana na magonjwa yasioambukiza.


Akizungumza baada ya kuhitimishwa na kupatikana wa mshindi Mgeni rasmi Mjumbe wa kamati ya Siasa CCM kata ya Mabwepande Amani Ngenje alisema kuwa mashindano hayo ni pamoja na vijana kujiandikisha katika uchaguzi wa Serikali ya Mtaa.

Kuandaa mashindano ni kufanya kuwafikia wananchi na vijana katika ushiriki wa jambo lolote kwa kutumia michezo.

Aidha amesema mashindano hayo yalishirikisha timu kumi ambapo nusu fainali zikapatikana timu mbili mbili na kuingia fainali timu mbili.

Hata hivyo amesema kuwa mashindano hayo yatakuwa endelevu katika michezo yote kwa kuanzia wameanza na mpira wa muguu.

Amesema katika michezo iliyofanyika kuna uwezekano kupata timu moja kwa uchaguzi kwa kila mchezaji.
Naye Mwandaji wa Mashindano yako Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbopo kata ya Mabwepande wilaya ya Kinondoni Ndugu Bushir Mziwandaalisisitiza umuhimu wa wananchi kufanya mazoezi kila mara ili kuboresha afya na kupunguza changamoto ya magonjwa yasiyoambukiza.



Mchezo ukiendela 























No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad