Na Mwandishi Wetu,DmNews tz online
MWENYEKITI wa Serikali ya mtaa wa Kibugumo katika Halmashauri ya Wilaya Kigamboni Yusuph Selemani Tindwa Amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wake amejitahidi kutatua Kwa kiwango kikubwa kero ya migogoro ya ardhi.
Amesema wakati anaingia madarakani mwaka 2019 mtaa wa kibugumo ulikuwa na changamoto kubwa ya ardhi lakini baada ya kuchaguliwa Yeye na wajumbe wake Kwa kushirikiana na mamlaka zingine ilikuwa ni kutatua migogoro hiyo.
Mwenyekiti Tindwa ameyasema hayo Leo Septemba 2, 2024 ofisni kwake mtaani humo wakati wa mahojiano maalumu na DmNews tz online .ambapo amesema Kwa kazi kubwa ambayo amefanya wananchi wa mtaa huo hasa wazee wanatamani kuona anaendelea kuwa kiongozi wa mtaa huo miaka mingine mitano.
Amesema licha ya changamoto hizo za ardhi lakini amefanikiwa kuimarisha eneo la elimu Kwa kujenga shule katika mitaa wake ,kuimarisha eneo la afya ,miundombinu ya barabara pamoja na Kuchangia ujenzi wa ofisi za Chama kwenye mtaa wa kibugumo na kidete.
No comments:
Post a Comment