Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani akizungumza na washiriki wa mafunzo ya waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki (BVR) watakaohusika na zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye Halmashauri ya Jiji la Dodoma, mkoani Dodoma Septemba 23,2024. Mzunguko wa tano wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utajumuisha mkoa wa Dodoma katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Halmashauri za Wilaya ya Bahi, Chamwino na Kongwa, mkoa wa Manyara katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu na Wilaya ya Kiteto na Simanjoro na mkoa wa Singida unaanza leo Septemba 25, 2024 hadi Oktoba mosi, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni. (Picha na INEC).
Tuesday, September 24, 2024
KAILIMA AZUNGUMZA NA WAENDESHA BVR DODOMA
Tags
# HABARI
# HABARI JAMII
HABARI JAMII
Labels:
HABARI,
HABARI JAMII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment