MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ametoa maelekezo wananchi waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerer (JNIA) kulipwa fidia zao.
Aidha DC Mpogolo, amezitaka kamati za wananchi hao wa Mtaa wa Kipunguni Kata ya Kipawa, Ilala, jijini Dar es Salaam, kufika ofisini kwake Septemba 17 kupewa maelekezo.
Ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za wanchi wa Kata za Minazi Mirefu, Kiwalani na Kipawa.
“Rais Dk Samia Suluhu Hassan, amesha toa maelekezo kwamba malipo yaanze kufsnyika. Kimachosubiliwa hivi sasa ni mifumo yanna gani malipo yaanze kufanyika,”alisema Mpogolo.
Aliwahakikishia wananchi hao wa Kipunguni wataanza kulipwa ndani ya Oktoba mwaka huu.
“Jumanne (Septemba 17 ) saa 2:00 asubuhi viongozi wa kamati waje ofisini wapate uhakika halafu watakuja kuwaambieni,”alieleza Mpogolo.
Kauli hiyo ilifanya mkutano kulipuka kwa shangwe huku wananchi hao wakiimba wimbo wa ‘Tuna imani na Samiia Oyaa! Oyaa! Oyaa’
Awali wananchi hao walicharuka, wakidai kuchoshwa na danadana za kulipwa fidia zao na kuwana pia viongozi wa CCM kulichukulia kwa uzito suala hilo kabla ya uchaguzi.
No comments:
Post a Comment