Morogoro 📍
Michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) imefunguliwa rasmi kuzikutanisha timu zinazowajumuisha watumishi wa serikali kutoka kwenye wizara, taasisi, wakala za serikali, ofisi za wakuu wa mikoa, halmashauri, pamoja na manispaa.
Uzinduzi huu umefanywa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko aliyeambatana na Naibu Waziri Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma pamoja Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Adam Malima.
Uwakilishi wa benki umeongozwa na Meneja wetu Mwandamizi wa Mahusiano ya Benki na Serikali, Josephine Kulwa, Meneja Mwandamizi Huduma za Kibenki kwa Serikali, Amanda Feruzi, pamoja na wafanyakazi wengine.
Friday, September 27, 2024
Home
Unlabelled
BITEKO AZINDUA MICHEZO SHIMIWI MKOANI MOROGORO
BITEKO AZINDUA MICHEZO SHIMIWI MKOANI MOROGORO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment