Tumezindua rasmi program yetu ya TUPO MTAANI KWAKO kupitia timu yetu bobezi ya mauzo. Sasa tunakufikia popote ulipo kupitia timu yetu ya mauzo kupata huduma zetu za kufungua akaunti , elimu ya mikopo pamoja na jinsi ya kutumia huduma zetu za kidijitali za VISA card, ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking. Program hiyo inaenda sambamba na kampeni ya Road show ya kutoa utambulisho kwa timu ya “Tupo Mtaani kwako” katika vitongoji na mitaa mbali mbali ya jiji la DSM Tupo Mtaani kwako, tukileta huduma kwa urahisi zaidi!
Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo Biashara Bw: Danford Muyango akizindua rasmi kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako” katika tawi la Kijitonyama, Letsya Tower
Baadhi ya Wafanyakazi wa ACB walioshirika katika uzinduzi wa program ya “Tupo Mtaani Kwako”
No comments:
Post a Comment