Katika kuhakikisha Watanzania wanapata bidhaa bora, Kampuni ya Denri Africa, inayoongoza kwa ubunifu katika utengenezaji wa mabegi yenye ubora wa kiwango cha juu imetangaza kufungua duka lake kubwa jipya jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa duka hilo huko Sinza Kijiweni na uliohudhuriwa na wadau mbalimbali, watu wenye ushawishi na waandishi wa habari, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Denri Afrika, Dennis Mwaura, alisema, "Upanuzi huu wa kusisimua unaashiria hatua muhimu katika dhamira yetu ya kutoa huduma bora kwa wateja wetu uzoefu wetu duniani.”
Kampuni ya Denri Afrika, Kwa mujibu wa Mwaura, ilichagua Tanzania kutokana na ukweli wa utamaduni na utendaji wake, wenye sifa ya kuwa soko kuu kwa kampuni yao.
"Ukuaji wa kasi wa tabaka la watu wenye kipato cha chini Tanzania na nafasi yake ya kimkakati Afrika Mashariki inaifanya kuwa muhimu sana kwa duka letu jipya. Tuna shauku ya kushirikiana na jamii ya Watanzania, kwa kuwapa fursa ya kipekee ya kupata bidhaa zetu bora na kuchangia katika uchumi wa ndani,” alieleza.
Alibainisha kwamba kuingia kwao nchini Tanzania kunaleta zama mpya ya ubunifu katika tasnia ya mifuko na kwamba duka lao litatoa mifuko ya viwango inayokidhi mahitaji mbalimbali.
Hatua hii ya kufungua duka Tanzania, Kwa mujibu wa Mtendaji huyo ni kufuatia mafanikio yao nchini Kenya, ambapo wanajivunia kuendesha matawi 13 nchini humo.
"Mabegi yetu yaliyotengenezwa kwa mikono kwa usahihi na uangalifu, yamekuwa ishara na mitindo bora, na kutufanya kuwa maarufu barani Afrika," aliongeza.
Kuhusu kile kinachowafanya kuwa tofauti na wengine, Mkuu wa Mauzo wa Kampuni ya Denri Afrika, Faith Mbutha, alifafanua, "Uendelevu ndio msingi wa shughuli zetu. Tumejitolea kutumia bidhaa ambazo ni rafiki kwa mazingira na kuwa na bidhaa inayodumu, na yenye ubora wa kiwango cha juu ambayo si tu kwamba inaonekana ni mizuri, bali pia ni rafiki kwa mazingira.”
Alifafanua zaidi kuwa wanajivunia miundo ya mabegi yao yanayoonyesha utajiri wa urithi wa utamaduni wa Afrika. "Tuna begi la Ankara la kusafiri ambalo linaonyesha mitindo mbalimbali ya kisasa na urembo wa kiutamaduni, kwa kuhakikisha kwamba bidhaa zetu zinakidhi mahitaji ya ndani, na ya kimataifa," alieleza.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa mauzo, wanaamini katika kukuza vipaji vya ndani na wameshirikiana na wasanii wa Tanzania kuleta ufundi wa kweli kwenye bidhaa zao, akiongeza kwamba ushirikiano huu si tu unasaidia uchumi wa ndani, bali pia unaongeza upekee wa bidhaa zao.
Baadhi ya vionjo katika ufunguzi huu ilikuwa kuonesha mabegi mbalimbalii, burudani mbashara na fursa ya kukutana na wabunifu walio nyuma ya Kampuni ya Denri Afrika.
Thursday, September 26, 2024
Home
Unlabelled
Baada ya kuvutiwa na utamaduni wa Tanzania, Denri Africa sasa yawekeza Dar
Baada ya kuvutiwa na utamaduni wa Tanzania, Denri Africa sasa yawekeza Dar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment