Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Chuo cha Ufundi Stadi (VET) Furahika kinatarajia kufanya mahafali Septemba 28 mwaka huu katika viwanja vya St.John Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi wa Mahafali hayo Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo hicho Dkt.David Msuya amesema kuwa wahitimu hao ni wale wanafunzi Elimu bure katika kuunga jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuwaandaa vijana kwenye ujuzi ili waweze kuzalisha.
Amesema kuwa katika jitihada hizo fani ya utalii asilimia 75 wameweza kuajirika kutokana na kuwaandaa vijana kwa weledi.
Amesema wanawapokea vijana kuanzia darasa la saba imekuwa ni faraja kutokana na kupata urahisi wa kuajirika huku akisifu sekta binafsi ya wamiliki wa hoteli kutoa kipaumbele kwa vijana hao.
Amesema kuwa Chuo hicho wanatarajia kwenda kutoa elimu ya ukatili kwa vijana Zanzibar.
Amesema kuwa mfumo walioanza nao wa elimu ya ukatili wa kijinsia ni kwenda katika mashina ya wajumbe ambapo huko ndio tatizo linakoanzia.
Amesema kuwa vijana wengi hawashiriki katika elimu mbalimbali kutokana na mazingira kuwa elimu hizo zinaanzia ngazi ya Kata hadi Taifa na kuacha kiini cha tatizo kwenye mashina.
Hata hivyo amesema kuwa wanawaomba wadau kujitokeza katika kutoa misaada mbalimbali ikiwemo magari hata kama mabovu watayatengeneza.
Amesema Taasisi hiyo wanafunzi wanatoa sehemu ya usajili wa mitihani yao kwa kiasi cha Sh.50,000 ambapo fedha hiyo chuo haipati kabisa.
Dkt.Msuya amesema kuwa kazi ya Serikali inafanya vitu vingi hivyo lazima tujenge mazingira kama wadau kutoa mchango wetu.
No comments:
Post a Comment