HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 11, 2024

ZIARA YA RAIS SAMIA MOROGORO YAWANG'OA WAPINZANI, 320 WAAMIA CCM, MBUNGE ABOOD AWAPOKEA.


IKIWA  ni siku chache Mkuu wa Nchi Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya Ziara kubwa ya Siku 5 Mkoani Morogoro kukutana na Wananchi, kuzindua Miradi mikubwa ya Maendeleo ikiwemo ya Viwanda, Madaraja, Barabara, maabara mtambuka, Majengo ya Chuo Kikuu Mzumbe n.k, Wapinzani Morogoro Mjini wameshindwa kuvumilia na kuamua kuamia Chama cha Mapinduzi.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abood amepokea wanachama wapya 320 kutoka Vyama mbalimbali vya Upinzani walioamua kwa hiari yao kujiunga na CCM mara baada ya kuridhishwa na Kazi nzuri inayofanywa na Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mapokezi hayo yamefanywa tarehe 11.08.2024 Katika Soko kubwa la Matunda na Mbogamboga (Soko la Mawenzi) wakati akizindua Shina walioanzisha wao la Wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi Mawenzi Sokoni.

Akizungumza nao, Mhe. Mbunge amewakaribisha kwa mikono miwili na kuwapongeza kwa maamuzi yao mazuri ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi uku akikubaliana nao kuwa Mhe. Dkt. Samia amefanya kazi kubwa Nchini na anaendelea kufanya kwa kishindo kikubwa kuwaletea Watanzania Maendeo, sambamba na hilo Mhe. Mbunge ameeleza upendo Mkubwa wa Dkt. Samia na kusema

"Mmeshuhudia Juzi Mhe. Rais alikuja Morogoro kututembelea, tumezungumza shida zetu na papohapo akazitatua, tumeomba hospitali ya rufaa katumwagia Bilion 5 palepale, tumemuomba maji mkataba wa bilioni 185 umecheleweshwa kusainiwa kamuelekeza Waziri mpaka oktaba mkataba usainiwe, tumemuomba pesa za barabara, amemuelekeza Waziri atuongezee, hivyo tuna kila sababu ya kumshukuru Rais wetu na ndio maana leo wenzetu uvumilivu umewashinda".

Aidha Mhe. Mbunge amewapongeza Wafanyabiara wa soko la Mawenzi kwa umoja wao na shughuli kubwa na nzuri wanayoifanya ya kulisha Morogoro na kushiriki katika ujenzi wa Nchi yao, vilevile ameahidi kuendelea kutatua kero na changamoto za soko hilo uku akibainisha alivyochonga barabara za soko hilo zilizokuwa kero kubwa kwa wafanyabiashara hao na kueleza mafanikio waliyoyapata baada ya kupata eneo hilo kutoka posta mpaka manispaa na sasa soko la kisasa labidi kujengwa.

Nae Katibu wa idara ya Uenezi Morogoro Mjini Ndugu Maulid Chamilila amewakaribisha kwa kishindo kikubwa wanachama wapya kutoka upinzani uku Diwani wa Kata hiyo Mhe Mbuguyu akieleza mafanikio yaliyofikiwa kwenye kata hiyo ikiwemo ujenzi wa Zahana n.k

Wanachama hao wapya kutoka katika vyama vya upinzani wameeleza furaha yao kujiunga CCM hasa wakielekeza shukurani zao kwa Mhe. Rais kwa kazi nzuri aliyoifanya na kuendelea kuifanya Nchini Kote.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad