Meneja wa TIC Kanda ya Kati Venance Mashiba akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi kwenye Banda la TIC katika Maonesho ya Kitaifa Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Meneja wa TIC Kanda ya Kati Venance Mashiba akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Banda la TIC katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma
Afisa Uwekezaji wa TIC Juma Nzima akizungumza na Wananchi Waliotembelea Banda la TIC kwenye Maonesho Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kinawaalika ,Wakulima, Wafugaji ,Wavuvi na wadau wote kutumia fursa katika maonesho ya Nanenane kujifunza uwekezaji.
Kauli hii imetolewa na Meneja wa Kanda ya Kati wa TIC Bw. Venanace Mashiba kwenye Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayofanyika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Bw. Mashina amesema kuwa TIC imeandaa taarifa na mbalimbali juu ya fursa zilizopo katika uwekezaji nchini hususani sekta ya Kilimo ,Mifugo pamoja na Uvuvi.
‘’Uwekezaji si suala watu wa nje kuja kuwekeza kwani Watanzania nao wanaweza kuwekeza. Amesema Mashiba
Mashiba ameongeza kuwa katika ukuaji wa Teknolojia TIC ina kituo cha kutoa huduma mahala pamoja katika kufanya usajili na huduma zingine zikiwemo na Taasisi za fedha.
Aidha amesema serikali ya awamu ya Sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan imefunguka kutokana na jitihada alizoweka katika kuvutia wawekezaji nje na ndani kutokana uzalishaji utaofanyika utakuwa na Masoko ikiwemo Kilimo ,Mifugo na Uvuvi.
"Maonesho ya Nane Nane ni fursa muhimu kwa wakulima na wananchi kupata taarifa za uwekezaji ambapo TIC itasimama bega kwa bega"amesema Mashiba
TIC iko katika kampeni ya kuhamasiha Uwekezaji wa ndani ambapo TIC inashiriki katika Kanda zote za Maonesho ya Nane Nane.
TIC inashiriki Maonesho ya Kilimo Nane Nane Kanda za Kusini Mbeya ,Kanda Ziwa Simiyu ,Kanda ya Kusini Lindi ,Kanda ya ya Kaskazini Arusha ,Kanda ya Mashariki Morogoro.
No comments:
Post a Comment