Na Albano Midelo
Vishikwambi hivyo vimekabidhiwa na Mwakilishi wa Taasisi hiyo, Dr. Joshua Mwakanyamale, kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Dr. Louis Chomboko, katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa mjini Songea.
Akizungumza kabla ya kukabidhiwa vishikwambi hiyo,Dr.Chombo amesema vishikwambi hivyo vimetolewa kwa ajili ya kusaidia kutekeleza afua ya toharakinga kwa wanaume ambayo inasaidia kuzuia maambukizi ya VVU kwa asilimia 60.
"Vishikwambi hivi vimekuja wakati muafaka na sasa vitaenda kugawiwa kwa vituo 43 kwa watoa huduma na waelimishaji rika ili kuweza kukusanya takwimu ya wale wote ambao tutakuwa tunawafikia kwa huduma ya tohara," amesema Dr. Chomboko.
Amebainisha kuwa Mkoa wa Ruvuma unashirikiana na Shirika la HJF -Medical Research International kwa ajili ya utekelezaji wa afua hiyo ili kuwezesha ufuatiliaji na kufikia wateja Zaidi ya 35,000 katika Mkoa ambapo hadi sasa wateja Zaidi ya asilimia 70wamefikiwa.
Naye Mwakilishi wa Shirika hilo ambaye pia ni Msimamizi wa Tohara katika Mkoa wa Ruvuma Dr.Joshua Mwakanyamale amesema Shirika hilo linafanya kazi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ikiwemo Mbeya,Rukwa,Songwe,Ruvuma na Katavi.
Dr.Mwakanyamale amesema vishikwambi hivyo vitarahisisha utunzaji wa taarifa kwani vinatumia mfumo na teknolojia ya kisasa wa kutunza kumbukumbu ambao ni rahisi zaidi tofauti na ule wa karatasi.
Amesisitiza kuwa vishikwambi hivyo vitawawezesha watoa huduma kuhifadhi taarifa kwa usalama zaidi na kuwezesha taarifa hizo kupatikana kwa urahisi zaidi pale zinapohitajika.
Ugawaji wa vishikwambi kwa watumishi wa umma katika Mkoa wa Ruvuma umekuwa endelevu ambapo serikali imeshatoa vifaa hivyo kwa Walimu wote wa Mkoa wa Ruvuma. Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Lous Chomboko akikabidhiwa vishikwambi 84 na Mwakilishi wa Shirika la HJF-Medical Reaserch International Dr.Joshua Mwakanyamale kwenye ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa mjini Songea.
No comments:
Post a Comment