HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 19, 2024

TASISI ZA UTATUZI WA MIGOGOZO KUKUTANA AGOST 22, 23, 2024 WAJIVUNIA KUBADILI MITIZAMO YA WAFANYABIASHARA

Makamu wa Raisi wa Taasisi ya Utatuzi wa Migogoro ya Kibiashara (TIArb), Aderickson Njunwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 19, 2024 katika kutoa elimu juu ya masuala ya utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala na mkutano mkuu utakaokutanisha watu zaidi ya 150.

KATIKA kuisaidia Mahakama Kupunguza Mrundikano wa Migogoro mahakamani, Taasisi ya Utatuzi wa Migogoro Tanzania ( TIArb) imeandaa mkutano utaojumuisha watu zaidi ya 150 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Mabara mengine.

Akizungumza leo Agosti 19, 2024 kuelekea mkutano huo, Makamu wa Raisi wa Taasisi ya Utatuzi wa Migogoro ya Kibiashara (TIArb), Aderickson Njunwa, amesema mkutano mkuu wa Usuluhisi wa migogoro ya Kiuchumi utakaofanyika Agost 22 na 23 Alhamisi na Ijumaa, 2024 jijini Dar es Salaam. 

Pia wiki ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kiuchumi itaanza kwa kutoa elimu kwa wananchi na jamii ijue nini taasisi hiyo inafanya katika jamii na wafanyabiashara wajue namna ya kutatua migogoro kwa njia mbadala bila kufika Mahakamani. 

Njunwa amesema kuwa mkutano huo utalenga kujadili usuluhishi wa migogoro ya sekta ya Ujenzi na migogoro ya uwekezaji wa kimataifa kwa njia ya mbadala. 

"Taasisi kama za kwetu zimekuwa na mchango mkubwa katika mataifa mengi na Tanzania yetu tunaona katika kuisaidia Mahakama kupunguza mrundikano wa  migogoro Mahakamani.

Tumekuwa na mahakama kama mdau mkuwa sana katika utatuzi wa migogoro kwa njia Mbadala." Ameeeleza Njunwa

Pia amesema ni  kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muunvano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika falsafa yake ya kimageuzi ya 4R ambayo ni sehemu inayowatia nguvu na kuwaelekeza kushughulikia migogoro ya kiuwekezaji kwa njia mbadala. 

"Lengo kuu la Mkutano huo utakao kutanisha wabobevu katika utatuzi wa  migogoro kwa njia mbadala wanaofanya migogoro hiyo na wanaofundisha namna ya kutatua migogoro hiyo lakini watu wote wenye kushughulikia migogoro na hata wafanyabiashara kwa lengo la kujadili usuluhishi wa migogoro ya usuluhishi na uwekezaji lakini hasa ni kutafuta kujengeana uwezo kwa wasuluhishi wetu na watendaji mbalimbali wanaohusika katika kusuluhisha hiyo mogogoro ya kijenzi pamoja na Uwekezaji kimataifa." Amesema

Pia watabadilishana Uzoefu katika eneo hilo la usuluhishi wa maigogoro kulingana na ukuaji wa kiteknolojia na mabadiliko ya sheria pamoja na mifumo mbalimbali  katika kishughulikia migogoro mbalimbali ya kibiashara pamoja na utatuzi wa migogoro. 

Pia watajadili changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika usuluhishi wa migogoro ili kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini. 

Kwa Upande wa Jaji wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara, Abdallah Ganzi,  amesema kuwa  Mahakama ya Tanzania  taasisi ya TIArb na nyingine za aina hii zipo kwaajili ya kuisaidia mahakama kutatua migogoro ya baina ya watu kwa njia mbadala. 

Licha ya kuwa migogoro lazima itokee katika jamii lakini lazima migogoro imalizwe ili jamii ipige hatua na iweze kuendelea na migogoro hiyo isipotatuliwa haitapiga hatua. 

"Kumekuwa na malalamiko na mashauri mahakamani yanachukua muda mrefu na sana, mingine gharama ni kubwa, wakati mwingine kesi inahitaji ujuzi zaidi wa kisheria hivyo pakiwa na taasisi mbadala inassidia jamii kuweza kumaliza migogoro kwa haraka zaidi na kwa gharama nafuu.

Amesema ili mtu yeyote aweze kupata haki kwa haraka hata kama hana ujuzi  mkubwa wa sheria lazima kuwepo na taasisi kama hiyo kwaajili ya kutatua migogoro inayojitokea katika miradi ya maendeleo.

Akizungumzia chanzo cha migogoro hizo jaji Ganzi amesema kuwa chanzo kikubwa ni katika Uandishi wa mikataba na kutokufuata vigezo na masharti kati ya taasisi au kampuni zilizokubaliana.

Pia ameeleza kuwa chanzo kingine cha migogoro namna sheria iliyochaguliwa katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya Uwekezaji na utekelezaji wa mirafi kusigana lakini amesema njia ya kuitatua ni namna nzuri ya kuandika mikataba kati ya pande mbili. 

Pia amesema wanjivunia taasisi kama hizo kusaidia wafanyabiashara kubadili mawazo yao juu ya utatuzi wa migogoro yao pasipo kufikia kuipeleka mahakamani. 

Mkutano huo utaangazia katika changamanoto na amna bora ya utatuzi wa migogoro ya Ujenzi na Uwekazaji wa kimataifa pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad