Mkuu wa Sehemu ya Maendeleo ya Mkonge wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Simon Kibasa akizungumza na wananchi Waliotembelea Banda la Bodi ya Mkonge Katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Mkuu wa Sehemu ya Maendeleo ya Mkonge wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Simon Kibasa akionesha wananchi bidhaa zinazotokana na zao la Mkonge wakati Waliotembelea Banda hilo kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
*Ya pili kwa uzalishaji Duniani
Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv
TANZANIA inaongoza kwa ubora wa Mkonge duniani na kuwa nchi ya pili kwa uzalishaji wa zao hilo duniani ambapo imezalisha tani 56,000 kwa kipindi cha mwaka 2023.
Akizungumza katika katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, Mkuu wa Sehemu ya Maendeleo ya Mkonge wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Simon Kibasa amesema mahitaji ya Mkonge duniani makubwa ikilinganishwa na kiasi kinachozalishwa.
Amesema Brazil ni nchi ya kwanza kwa uzalishaji lakini Tanzania inaipita kwa ubora kutokana na kuwa na mitambo ya kisasa katika kuchakata mkonge.
"Uzalishaji wa Mkonge upo katika mikoa 16 ambapo Bodi inaendelea kuhamasisha wananchi kuingia katika kilimo hicho kutokana na kuwepo kwa soko kubwa katika soko la Dunia.
"Mahitaji ya soko la mkonge ni tani Milioni mbili ambapo wananchi wakiingia katika kilimo hicho Tanzania itaongoza kwa uzalishaji na ubora zaidi ya sasa," amesema.
Aidha kiwango cha uzalishaji duniani 600,000 hivyo kunafanya soko hilo kuelemewa hatuaà yanayotokana mahitaji kuwa makubwa.
No comments:
Post a Comment