Kaimu Kamanda TAKUKURU Mkoa wa Pwani Ally Sadiki akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo pichani leo Agosti 13,katika Ukumbi wa mikutano ofisini hapo.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiendelea na majukumu yao kwenye mkutano huo
Na Khadija Kalili Michuzi Tv
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Pwani wamesaidia kuokoa kiasi cha Bil.1 ,688,289,634.09 katika kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu.
Yamesemwa hayo leo Agosti 13 na Kaimu Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Ally Sadiki amesema TAKUKURU ilifanya uzuiaji katika ukusanyaji wa mapato upande wa ushuru wa huduma katika Halmashauri ya Mji Kibaha na kufanikiwa kukusanya kiasi hicho cha fedha ambazo awali zilikua zinapotea kwa baadhi kwa baadhi ya watumishi kushindwa kufuata sheria,kanuni na utaratibu za ukusanywaji wa mapato upande wa ushuru wa huduma.
"Katika ufuatiliaji huo TAKUKURU imebaini kuwa baadhi ya watumishi wa Halmashauri Kitengo cha ukusanyaji wa mapato kuwa kuwa na via sheria vya uvunjifu wa maadili kwa kushindwa kuwajibika
katika ufuatiliaji nanukusanyaji wa ushuru wa huduma.
Amesema kuwa baadhi ya watumishi kuingia makubaliano na wafanyakazi katika kulipa ushuru wa huduma na kuwaruhusu kulipa kiasi kidogo ukilinganisha na mauzo yao halisi.
Baadhi ya Wafanyabiashara wanapotaka kulipa ushuru wa huduma wanajikadiria mauzo yao hivyo kusababisha kulipa ushuru wa huduma kiasi kidogo ukilinganisha na mauzo halisi kutoka kwenye Z-REPORT kama sheria inavyowataka kutumia Z-REPORT katika kukokotoa mauzo"amesema Kaimu Kamanda TAKUKURU Sadiki.
Amefafanua kwa kusema kuwq baadhi ya Wafanyabiashara kulipa nusu au hawalipi kabisa ushuru wa huduma kwa madai kwamba Kibaha ni eneo la uzalishaji
(Viwanda) na siyo eneo la mauzo (Sokoni), hii ni kutokana na wafanyakazi kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na malipo ya ushuru wa huduma huku baadhi ya Wafanyabiashara wamegundulika kuwa wanamiliki mashine za EFD zaidi ya moja hivyo kuficha zingine ili kukwepa kulipa kiasi sahihi anachotakiwa kukilipa.
Kaimu Kamanda TAKUKURU Mkoa wa Pwani Sadiki ameongeza kwa kusema kuwa taasisi hiyo imesaidia kuongeza makusanyo hayo baada ya kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha baada ya kuonekana mapato yaliyokusanywa awali kwa robo ratu za mwanzo kwa mwaka wa fedha kati ya 2023 na 2024 ni ndogo kulingana na vyanzo vya mapato vilivyopo ndani ya Halmashauri.
"Katika kipindi tajwa tumefanya uchambuzi wa mfumo mmoja katika eneo la ukataji wa kodi ya zuio katika miradi ya maendeleo Halmashauri ya Kibiti" amesema Kaimu Kamanda TAKUKURU Mkoa wa Pwani Sadiki.
Aidha kwa upande wa ufuatilia wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo tayari wamefuatilia.kiradi kumi yenye thamani ya Bil.10,619,073,893.77 katika sekta za Elimu, Maji,TANESCO, Afya,Ujenzi ,barabara na biashara kati ya miradi hiyo hakukuwa na mradi ulioonekana kuwa na mapungufu.
Wakati huohuo TAKUKURU Mkoa wa Pwani imeendelea na utekelezaji wa program ya TAKUKURU Rafiki na kuzifikia kata sita huku kero zilizoibuliwa na kupatiwa ufumbuzi zimetoka Idara ya Jeshi la Polisi, Utawala ,Afya , Elimu,Ardhi,TANESCO na Barabara.
Kaimu Kamanda Sadiki amesema kuwa katika kipindi taja juu wamepokea malalamiko 95 huku kati ya hayo malalamiko 55 yamehusu rushwa na taaifa hizo zimeshughulikiwa kwa mujibh wa sheria kwa kuanzia uchunguzi ambao upo katika hatua mbalimbali za uchunguzi.
"Taarifa 40 zilizobaki ambazo hazikuhusu rushwa zimeshughulikiwa kwa njia ya uelimishaji,uzuiaji ushauri nankuhamishiwa idara nyingine, taarifa hizo zimepokelewa kwa Mchanganuo ufuatao TAMISEMI 22,Mifugo/Uvuvi3,Elimu 14,Polisi7,Ardhi12,Fedha3,Maji2,Mahakama 5,binafsi9, Ujenzi6,Afya7,
Siasa moja,Manunuzi moja,Maendeleo ya jamii moja,Kodi/ Mapato moja.
Katuka kipindi hiki TAKUKURU Mkoa wa Pwani imefungua jumla ya kesi mpya 11 Mahakamani huku kesi saba wametiwa hatiani.
Akizungumzia kuhusu namna walivyojipanga na vitendo vya rushwa katika uchaguzi, "Mkoa wetu una ofisi tisa katika Wilaya zote kuna jumla ya Kata 133,Mitaa 490 na Vitongoji 2029, kwa kipindi hiki tumeshaanza kufanya ufuatiliaji wa vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika baadaye mwaka huu".
Mwisho Kaimu Kamanda Sadiki ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani kuendelea kuunga mkono jitihada za kufichua vitendo vya rushwa na wala rushwa kwa kutoa taarifa sahihi zitakazowezesha kuwachukulia hatua wahusika hasa katika kipindj hiki tunapoelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na amewasisitizawananchi waonunua maeneo wahusishe serikali za mitaa na kufuata sheria na kanuni na taratibu ili kuepusha migogo ya ardhi inayojitokeza mara kwa mara na kwenda na kauli mbiu isemayo kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu tutimize wajibu wetu.
No comments:
Post a Comment