-Balozi Kingu ashauri Wakandarasi wazawa kufikiria kufanya Miradi nje ya nchi
-Mhandisi Hassan Saidy asisitiza REA itaendelea kuwaunga mkono Wakandarasi wanaofanya vizuri tu si vinginevyo
Wakala wa Nishati Vijijini (REA), leo tarehe 24 Agosti, 2024 imewapa tuzo na vyeti maalum Wakandarasi waliofanya vizuri kupitia Mradi wa Kupeleka Umeme maeneo ya Pembezoni mwa Miji Awamu ya Tatu (Peri Urban III) kote nchini ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora unatakiwa.
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi, Hassan, Saidy alisema utendaji madhubuti (Performance) na kukamilisha Miradi ya PERI Urban III kwa wakati kumechangia Wakandarasi hao kupewa tuzo hizo.
“Kipekee, niwapongeze Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kuwasimamia Wakandarasi wazawa kwenye Miradi ya PERI Urban III na kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati. Natambua kuwa ninyi ndio mlio kuwa Washauri Elekezi wa mradi huu, hivyo mnao mchango mkubwa katika mafanikio haya”. Amekaririwa Mhandisi Saidy.
Mhandisi Hassan Saidy amesema kuwa REA iliahidi kuwa kwa sasa, itaanza kuwatunuku tuzo na vyeti kwa Wakandarasi wanaofanya vizuri kwenye usambazaji wa nishati ya umeme vijijini.
“Tuliahidi na sasa tumetimiza, tumeona hii ni njia nzuri ya kuwafanya waongeze nguvu, kwenye utekelezaji wa Miradi ya usambazaji wa nishati ya umeme vijijini, wale wanaofanya vizuri basi tuwatambue”. Amesisitiza Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi, Hassan Saidy.
Naye, Mgeni Rasmi wa hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Mhe. Balozi na Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu amewapongeza Wakandarasi hao kwa kumaliza kwa wakati na kwa ubora.
“Kumbukeni kuwa, juhudi zenu zina mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa letu, na kwa hivyo, endeleeni kujitolea kwa moyo ili kuhakikisha miradi yote, mliyopewa inakamilika kwa wakati.” Amesisitiza, Mhe. Balozi Kingu.
Naye Mkurugenzi wa Umeme Vijijini (DRE) kutoka REA, Mhandisi, Jones Olotu amesema hafla ya kuwapa tuzo Wandarasi hao umelenga kuwakumbusha na kuhusu wajibu wao wakati wa utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa nishati vijijini pamoja kutambua juhudi zao kwenye maendeleo ya Sekta ya Nishati nchini.
Wakandarasi waliofanya vizuri na kutunukiwa tuzo na vyeti ni pamoja na kampuni kwanza ni ya DIEYNEM Co Ltd, kampuni ya pili ni DERM Group (T) Ltd, kampuni ya tatu ni Central Electricals & Electronics International Ltd na kampuni ya nne ni OK Electrical & Electronics Services Ltd, kampuni zote hizo ni za Watanzania.
Maeneo ya utekelezaji wa Miradi ya Kupeleka Umeme maeneo ya Pembezoni mwa Miji Awamu ya Tatu (Peri Urban III) sambamba na Wakandarasi hao ni kama ifuatavyo: - kampuni ya DIEYNEM Co Ltd (Lot 2, mkoani Kagera); kampuni ya DERM Group (T) Ltd (Lot 4, mkoa wa Mbeya & Lot 5, mkoa wa Mtwara); Central Electricals & Electronics International Ltd (Lot 6, mkoa wa Singida) na mwisho OK Electrical Services Ltd (Lot 7, mkoa wa Tabora na Lot 8, mkoa wa Tanga).
Naye Mwakilishi kutoka Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB); Mhandisi, Gloria Simbakali ameipongeza REA kwa kuwaalika ili kushiriki hafla hiyo lakini pia amepongeza kwa hatua ya utoaji wa tuzo kwa Wakandarasi waliofanya vizuri kwa jukumu moja wapo la CRB ni kuratibu zoezi la usimamizi pamoja na uwajibikaji (Performance) kwa Wakandarasi (Wanachama).
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO); Mhandisi, Robert Semsela ameipongeza REA kwa kutekeleza na kuendelea kuwafikia Wananchi wengi kupitia Miradi mbalimbali ya kusambaza umeme vijijini na kuongeza kuwa lengo ni kuboresha maisha ya Watu wa vijijini.
Naye, Mhandisi, Ridhuan Mringo, Mwenyekiti wa DERM Group ameipongeza Serikali kupitia REA kwa kutenga fedha za kutosha kwenye miradi ya kusambaza umeme vijijini mkubwa.
“Tunaishukuru Serikali kwa kuwa tunalipwa katika muda muhafaka kwa kila madai yetu ambayo ni halali na yamekidhi vigezo”. Alikaririwa, Mhandisi, Mringo.
Saturday, August 24, 2024
Home
Unlabelled
REA YAWAPA TUZO WAKANDARASI WALIOFANYA VIZURI MIRADI YA PERI URBAN III
REA YAWAPA TUZO WAKANDARASI WALIOFANYA VIZURI MIRADI YA PERI URBAN III
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment