RAIS wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi atembelea banda la TADB katika Maonesho ya Saba ya Kilimo "Nane Nane" 2024, Dole Kizimbani – Unguja.
Rais Mwinyi ametembelea banda hilo alipokuwa akifungua rasmi maonesho ya saba ya Kilimo (nane nane) Zanzibar tarehe 3/8/2024.
Katika banda la TADB Mhe. Dkt. Mwinyi amepokelewa na Kaimu Meneja wa Kanda ya Zanzibar, Bw. Michael Madundo na kupatiwa muhtasari wa maendeleo ya benki ikiwemo taarifa ya utolewaji wa mikopo, idadi ya wanufaika wa mikopo ya benki Zanzibar pamoja na:
✅️ Jitihada zinazofanywa na benki katika kutoa elimu ya fedha na kilimo biashara Zanzibar
✅️ Mendeleo ya Mradi Shirikishi wa Wasindikaji, Wazalishaji wa Maziwa Tanzania (TI3P) ndani ya Zanzibar
✅️ Maendeleo ya Mfuko wa Dhamana wa Wakulima Wadogo (SCGS)
🟢 Mhe. Dkt. Mwinyi pia alipata nafasi ya kuona kazi za wanufaika wa TADB ikiwemo Kampuni ya Bin Mwewe wakulima wa Matunda na mbogamboga, Shemsa Taraba na Kampuni ya MPF wafugaji wa kuku wa mayai.
No comments:
Post a Comment