Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye Banda la NHIF wakati alipotembelea Maonesho Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu,
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kuhakikisha wanawafikia wananchi wote ili wawe ndani ya mfumo wa Bima ya afya.
"Nataka bima kwa watu wangu wote, nitawaita tuzungumze" alisema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ameyasema hayo leo wakati akitembelea maonesho ya Nane Nane kitaifa mkoani Dodoma.
Hivi karibuni Mhe. Rais akiwa ziarani mkoani Katavi na Rukwa kwa nyakati tofauti alihamasisha wananchi kukata Bima ya afya ili wawe na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wote.
No comments:
Post a Comment