Mbunge wa Viti Maalum UWT (watu wenye ulemavu) Stella Ikupa akikabidhi mashuka katika hospitali ya Wilaya ya Ubungo Kimara jijini Dar es Salaam leo Agosti 06, 2024.
Mbunge wa Viti Maalum UWT (watu wenye ulemavu) Stella Ikupa akikabidhi mashuka katika Kituo cha Afya cha Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Agosti 06, 2024.
MBUNGE wa Viti Maalum UWT (watu wenye ulemavu) Stella Ikupa, leo Agosti 06, 2024 amekabidhi mashuka 41 katika kituo cha Afya Kinondoni, na hospitali ya Wilaya ya Ubungo iliyopo Kimara kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akikabidhi mashuka hayo kwa uongozi wa Idara ya Afya ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, Ikupa amesema ni zawadi maalumu kutoka kwa Rais Dkt. Samia ambayo ametupatia wabunge tuje tuwaleteni.
Amesema, Rais Dkt. Samia, amekuwa mstari wa mbele kuboresha sekta ya afya hivyo kuwataka watumishi kutekeleza majukumu yao kwa kuwahudumia wananchi kwa moyo wa upendo.
“Hii kazi ya afya ni ya Mungu, mnavumilia mengi lakini endeleeni kuhudumia wananchi kwa moyo huo." Amesema Stela
Pia lisisitiza, kutengwa kwa vyumba maalumu kwaajili ya kujifungulia watu wenye ulemavu pamoja na vitanda maalumu.
“Kila anaejifungua anahitaji chumba cha siri lakini watu wenye ulemavu, wasioona pamoja na Wasiosikia wanaojifungua wanahaji chumba cha siri zaidi na vifaa maalumu ikiwa ni pamoja na kitanda cha kujifungulia.”
Akizungumza alipofika katika hospitali ya Ubungo Stela amesema kuwa watu wenye mahitaji maalumu wanahitaji uangalizi tofauti ukilinganisha na watu wengine hivyo amewaomba Madaktari na wauguzi kutowanyanyapaa watu hao kulingana na uhitaji wao.
Kwa upande wa Kituo cha afya cha Kinondoni, Stela amewapongeza kwa kutenga chumba maalumu kwa watu wenye ulemavu wanaofika kunifungua na pia ameahidi kutoa msaada wa kitanda maalumu kwaajili ya kusaidia watu wenye ulemavu.
Akipokea mashuka hayo, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Peter Nsanya, amemshukuru Rais Dkt.Samia na mbunge huyo kwa msaada wa mashuka hayo ambapo amesema yamewafikia Kwa muda muafaka.
“Kwa kweli tunamshukuru sana Rais Dkt. Samia, kwa namna anavyoboresha sekta ya afya.
Ukitazama kituo hiki majengo yake unaweza kudhani ni hospitali kubwa na huduma muhimu zote zinapatikana hapa.” amesema Dkt.Nsanya.
Katika hatua nyingine, Mbunge Ikupa amekabidhi mchango wa viti 200 kwa uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Kinondoni na Wilaya ya Ubungo huku akisisitiza kutangaza maendeleo mazuri yaliyofanywa na Rais Dkt. Samia.
“Tangu Rais Dkt. Samia, aingie madarakani, hakuna mradi uliosimama. Kuweni majasiri. Tembeeni kifua mbele kuwaeleza wananchi maendeleo hayo.” ameeleza Ikupa
Stela amesisitiza kuzisemea kazi zinazofanywa na Rais Dkt Samia, kutampa moyo wa kufanya kazi kubwa zaidi hususan miradi mikubwa ya kimkakati iliyotekelezwa na Rais na kutekeleza Ilani ya CCM.
“Nimetoa mchango huu wa viti hivi 200 katika Wilaya ya Kinondoni na viti 360 katika Wilaya ya Ubungo vitagawiwa katika ofisi za UWT katika kata zote za wilaya ya Kinondoni,na Ubungo." Amesema Stela
Lengo ni kuandaa mazingira bora ya utendaji kazi wa UWT kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utaofanyika mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani.
Pia Stela amewaomba UWT kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura, kugombea nafasi na kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.
Tuwahamasishe wanachahama wetu kugombea nafasi za uongozi na siku ya kupiga kura, kuhakikisha wenye viti wetu wa serikali za mitaa wanashinda. " Ameeleza Stella
Akizungumza kuhisiana na Mikopo MBUNGE Stela amesema mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa vikundi vya wajasirimali wanawake, vijana na wenye ulemavu, iko tayari na muda wowote itaanza kutolewa.
Kwa upande wa Katibu wa UWT Wilaya ya Kinondoni, Aziatu Salumu Juma, amemshukuru Mbunge huyo kwa msaada huo viti ambao utasaidia kuboresha huduma katika ofisi zao.
Amesema, mbali na msaada huo, ikupa aliwahi kukabidhi kompyuta katika ofisi za UWT na kwamba msaada wake umekuja kipindi kuafaka vikao vikiendelea kusaka ushindi wa CCM.
Akiwa katika hospitali ya Wilaya ya Ubungo, Stela amesema atawasilisha changamoto walizomueleza Kwa Rais Dkt. Samia ili ziweze kutatuliwa Kwa wakati na kuondokana na changamoto wanazopitia katika hospitali hiyo.
MBUNGE WA VITI MAALUM UWT (WATU WENYE ULEMAVU) STELLA IKUPA ALIPOKUWA KATIKA OFISI ZA WILAYA YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM LEO AGOSTI 06, 2024.
MBUNGE WA VITI MAALUM UWT (WATU WENYE ULEMAVU) STELLA IKUPA ALIPOKUWA KATIKA OFISI ZA WILAYA YA UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM LEO AGOSTI 06, 2024. KWAAJILI YA KUGAWA VITI VYA KATA ZA WILAYA HIYO.
MBUNGE WA VITI MAALUM UWT (WATU WENYE ULEMAVU) STELLA IKUPA ALIPOKUWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA UBUNGO, KIMARA. KWAAJILI YA KUGAWA MASHUKA.
No comments:
Post a Comment