HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 25, 2024

MAONESHO YA 7 YA KITAIFA YA TEKNOLOJIA YA MADINI YANATARAJIWA KUFANYIKA TAREHE 2 MWEZI OKTOBA - GEITA



Maonesho ya SABA ya Kitaifa ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanatarajiwa kuanza Mwezi wa OKTOBA Tarehe PILI Mjini GEITA ambapo wafanyabiashara wametakiwa kuendelea kuwekeza katika malazi ili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa GEITA iwe na maandalizi ya uandaaji wa matukio makubwa ili Viongozi wa Kitaifa na Kimataifa wapate maeneo ya malazi.



Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa GEITA HASHIM KOMBA amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa Hoteli ya Mazinzi Mjini Geita na amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa serikali ya Mkoa wa Geita inapenda kufanya Mkoa wa GEITA kuandaa mikutano,matamasha na maonesho mbalimbali lakini sehemu za malazi kwa viongozi wakubwa bado ina changamoto.

KOMBA amesema kwa sasa Serikali imetoa zaidi ya Shilingi BILIONI ISHIRINI NA MBILI kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami KILOMITA KUMI NA SABA maeneo ya Mjini Geita kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Mji huo na kuwavutia wawekezaji.



Mkurugenzi wa Hoteli ya Mazinzi LUCAS MAZINZI ameiomba serikali kuendelea kushirikiana na wawekezaji ili wawekezaji waendelee kuwekeza zaidi katika maeneo mbalimbali kuanzia maeneo ya malazi na vyakula nk.



Msoma lisala katika Ufunguzi wa Hoteli hiyo COSTANTINE MAZINZI amesema hoteli hiyo ilianza ujenzi mwaka 2019 hadi kukamilika mwaka huu imegharimu Shilingi MILIONI MIA NANE na lengo la uwepo wa hoteli hiyo ni kwa ajili ya kupendezesha Mji wa Geita pamoja.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad