HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 12, 2024

KONGAMANO LA WATU WENYE ULEMAVU LAFANYIKA DAR, MBUNGE STELA IKUPA KUENDELEA KUWATETEA

 

Mbunge wa Viti Maalum UWT (watu wenye ulemavu), Stella Ikupa  kulia akizungumza na watu wenye ulemavu katika kongamano lililofanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 12, 2024.
MBUNGE wa Viti Maalum UWT (watu wenye ulemavu), Stella Ikupa leo Agosti 12, 2024 ameandaa kongamano la Watu wenye ulemavu wanaoishi katika jijini Dar es Salaam akiwa na lengo la kuwakutanisha pamoja ili kujadili changamoto na fursa zilizopo nchini.

Kongamano hilo lilitawaliwa na mada mbalimbali pamoja na maswali na majibu kutokana na changamoto wanazozipitia watu wenye ulemavu nchini.

Akizungumza kuhusiana na mambo mbalimbali ambayo serikali imeshayatatua ambayo yalikuwa kikwazo kwa watu weye ulemavu, Stela amesema kuwa tayari serikali imesikia kilio cha watu wenye ulemavu kwa kuandaa miundombinu rafiki inayoweza kutumiwa katika majengo na mahali panapopatikana huduma za kijamii kama husipitali, Masoko na Vituo cha Daladala na mashuleni.

Stela amesema ataendelea kuzisemea na kutetea changamoto za watu wenye ulemavu ili kuhakikisha serikali inazitafutia uvumbuzi.

"Mimi kama mwakilishi wa kundi la watu wenye ulemavu bungeni, nimekuwa mstari wa mbele kuzisemea changamoto za kundi la watu weye Ulemavu pia nafurahishwa na hatua zinazochukuliwa na serikali katika kuzitatua." Amesema Stela

Pia ametolea mfano tatizo la uchache wa walimu wenye taaluma na uwezo wa kufundisha kundi hilo na kwamba tayari serikali imeshaanza kulifanyia kazi kwa kuweka mikakati ya kuhakikisha vyuo vinafundisha lugha ya alama na elimu ya wenye uhitaji maalumu.

"Serikali imesikia maombi yetu na inayafanyia kazi, muda si mrefu tutakuwa na wataalamu wa kutosha wa kufundisha kundi hili, tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulifanyia kazi hili. Ameeleza .

Amesema sio kwenye elimu pekee lakini pia na kwenye sekta ya afya, serikali imetusikia inafanyika kazi, kwa hiyo tushukuru kwa hatua hizi zinazochukuliwa na serikali tunaamini itaendelea kufanyia kazi changamoto zetu zote tuwe wavumilivu."

Stela kwa upande wa Mikopo kwa watu wenye ulemavu amesema kuwa mikopo ipo tayari wakae mkao wakula baadhi ya taratibu ndogo zikikamilika wataelekezwa ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na serikali.

Akizungumzia kuhusiana na uchaguzi wa Serikali ya Mtaa Oktoba na Uchaguzi Mkuu wa 2025, Stela amewaomba wajitokeze kujiandikisha pamoja na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi pia wajitokeze kwenda kupiga kura wakati utakapofika.

Kwa Upande wa Mtoa mada kuhusu sheria, Mwansheria, Gidione Mandesi amewaomba watu wenye ulemavu wasiwe nawoga pale wanapotaka kwenda mahakama kueleka mashtaka yao.

"Niwatoe wasiwasi kwa watu wasio na uwezo wakumlipa mwanasheria wa kuwatete, huduma hiyo ni bure kwa watu wasio na uwezo wa kulipa.

Pia Mandesi amewaasa watu wenye ulemavu kuwa na ushirikiano, waweze kutafuta taarifa, kupendana na kutokuwekeana kauzibe pale zinapotokea fursa mbalimbali ili kila mmoja aweze kujua kinachoendelea

Kongamano hilo lilikusanya walemavu kutoka wilaya zote za jijini la Dar es Salaam, madiwani pamoja na wadau mbalimbali kutoka Takwimu, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), TWAWEZA, Kituo cha Haki za Binadamu(LHRC), LSF, na UNWomen na kufadhiriwa na ITF, Eulopean Union, FCS, TCRA, TAKWIMU na Cokacola.








Baadhi ya watu wenye ulemavu wakiwa katika kongamano jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad