Sehemu ya mtambo wa kutengeneza Asali.
Na Chalila Kibuda ,Dodoma
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ufugaji Nyuki ya Igembensabo farm implements LTD na chamwino Beekeepers Honey Processing Plant Mazari Taji amesema kuwa Soko la Asali limekuwa kubwa ndani na nje ya nchi hivyo kunahitajika jitihada zaidi za kuendelea kuvuna Asali kisasa.
Mazari aliyasema hayo katika kiwanda chake kilichopo ndani ya Maonesho ya Nane Nane Nzuguni Jijini Dodoma,amesema kuwa Mamlaka zinazohusika katika kutoa vibali kuwa na dawati moja kuondoka na msululu WA makaratasi ya kufuata kila Ofisi.
Amesema kuwa kuendelea na kuwepo na kufuata taratibu katika kila Ofisi kuna sababisha kuwepo kwa njia ya panya katika usafirishaji wa Asali katika soko la ndani.
Hata hivyo amesema kuwa katika Viwanja vya ndege mtu akiwa na galoni ya Lita tano apite tu kwani anakwenda kuitangaza nchi kwani vikwazo wanayopata abiria wanakwenda na asali nje ya nchi haileti Afya.
Aidha amesema kuwa bidhaa za mizinga zinatokana na mbao ambazo sio Mali asili ambapo baadhi ya Mamlaka kuwakamata kigezo kuwa ni mali asili.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa wakati wa usafirishaji wa Asali wanahitaji kupata namba ya Gari inayobeba asali hali hiyo kwa Wafugaji wadogo hawawezi kumudu katika umiliki wa Gari.
Amesema katika utendaji wa kampuni inawafindisha Wafugaji wa nyuki pamoja na kuwapa mizinga na wanauza katika kampuni hiyo wanatoa mirabaha kwa Wafugaji hao.
Hata hivyo amesema serikali imeweka mazingira mazuri katika Ufugaji wa nyuki hivyo Mamlaka kuangalia namna ya kuwasaidia na sio kuwadidimiza
No comments:
Post a Comment