Gavana wa Jimbo la Haut-Katanga, Jacques Kyabula (katikati) akimkabaizi mfano wa hundi yenye thamani ya Dola za Marekani 50,000 Waziri wa Afya, Joseph Nsambi Bulanda wa Haut-Katanga (watatu kulia), zilizokusanywa katika CRDB Bank Marathon Congo iliyofanyika leo Agosti 4 2024 katika jiji la Lubumbashi DRC. Wengine pichani ni Balozi wa Tanzania nchini DRC, Said Mshana (wapili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Kundi la Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (watatu kushoto), Mwenyekiti wa Bodi wa CRDB Bank DRC, Dkt. Fred Msemwa (wapili kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Benki ya CRDB, Bruce Mwile (wakwanza kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank DRC, Jessica Nyachiro.
Lubumbashi – CRDB Bank Marathon imefanyika leo kwa mara ya kwanza nje ya mipaka ya Tanzania katika jiji la Lubumbashi ambapo zaidi ya wakimbiaji 1,000 wameshirikina kufanikisha lengo la kukusanya USD 50,000 kwa ajili ya kusaidia wodi ya watoto katikaHospitali ya Jason Sendwe.
Mgeni rasmi katika mbio hizo ambazo zimewekahistoria katika marathon ambazo zimewahikufanyika katika jiji la Lubumbashi alikuwa ni Gavana wa Jimbo la Haut-Katanga Mhe. Jacques Kyabula ambaye aliambatana na mawaziri 10 wa Jimbo hilo wakiongozwa na Waziri wa Michezo, pamoja na Waziri wa Afya.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mbiohizo za hisani zilizobeba kaulimbiu isemayo‘Tabasamu Limevuka Mipaka’ Gavana Kyabulaameipongeza Benki ya CRDB kwa kuwaletapamoja WaCongo pamoja na washiriki kutoka mataifa ya jirani kuja kuchangia kuboreshahuduma za afya kwa watoto na kukuza ustawi wa jamii.
"Tunaishukuru CRDB Bank Marathon kwa kusaidia jitihada za Serikali kuboresha huduma za afya kwa wananchi. Serikali yetu inatoakipaumbele kikubwa katika afya, na tunafurahishwa na jitihada zinazofanywa na Benki ya CRDB katika kusaidia kuboresha afyaya watoto," alisema Gavana Kyabula.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchiniDRC, Balozi Said Mshana aliipongeza Benki ya CRDB kwa juhudi zake za kukuza mahusianoya kimataifa na kuimarisha umoja na mshikamano katika jamii. Balozi Mshanaalisema mbio hizo zilizozaliwa Tanzania zinaonyesha ubunifu ambao taasisi za kitanzania zinaweza kupeleka nje ya nchi katikakusaidia kukuza ustawi wa jamii.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Bank DRC, Dkt. Fred Msemwa alieleza kuwa marathon hiyoni sehemu ya mkakati wa Benki kusaidia juhudiza serikali katika kukuza ustawi wa watu wa Congo. "Marathon hii si tu inahamasishamichezo, bali pia inajenga utamaduni wa kujitolea kwa jamii.
Benki yetu inaamini kwa kuwaleta watu pamoja tunaweza kuyafikiamakundi mengi kwa urahisi na hivyo kukuza ustawi wa jamii kupitia programu bunifu kama CRDB Bank Marathon, lakini pia kupitia huduma na bidhaa zetu bunifu tutaweza kusaidia jitihadaza kukuza ujumuishi wa kifedha na kiuchumi," alisema.
Akitangaza matokeo ya mbio hizo, MkurugenziMtendaji wa CRDB Bank Congo, Jessica Nyachiro, aliwashukuru washirika wa mbio hizoAfricell, Orange, Ogowe Cleaning, Kin Marche, Policlynique Delta, Shalina, Vinmart Foundation, SUNU Insurance, na Dukan. “Pamoja na kuwahuu ni mwaka wa kwanza kwa mbio hizi lakinimwitikio umekuwa mkubwa sana. Tunawashukuru sana washirika wetu na wakimbiaji wote mlioungana nasi kusambazatabasamu kwa watoto.”
Marathon iliyofanyika leo Lubumbashi ni ya kwanza kati ya tatu ambazo zimepangwakufanyika mwaka huu nchini DRC, Burundi, na Tanzania. Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation ambao ndio waandaji wa mbio hizo, Tully Esther Mwambapa ameeleza furaha yakebaada ya mbio hizo zilivyopokelewa vizuri sana nchini DRC.
Tully amewashukuru Watanzania ambaowamejitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo za DRC ikiwamo kuwashukuru washirika wakuu wa mbio hizo Sanlam, CRDB Insurance Company, na Clouds Media. "Nitumie nafasi hiikuwakaribisha watu wote kuendelea kujisajilikwa mbio za Burundi tarehe 11 Agosti na Tanzania tarehe 18 Agosti," aliongezea.
Papy Kayombo, mshindi wa mbio za Kilometa21 katika CRDB Bank Marathon Congo, ameeleza furaha yake ya kushiriki katika mbiohizo na kusema ushindi wake ni sehemu ya kusambaza tabasamu kwa watoto ambaowatapata matibabu katika hospitali ya Jason Sendwe.
Kayombo alisema, "Katika jiji la Lubumbashi utamaduni huu ni mpya na ninaonautasaidia sana kujenga mshikamano katikajamii. Naipongeza sana Benki hii yetu ya CRDB, imeonyesha upendo mkubwa sana kwa watotowetu na sisi tunaahidi kuiunga mkono."
Viongozi hao pia waliambatana na Balozi wa Tanzania nchini DRC, Balozi Said Mshana, Balozi wa Burundi nchini DRC, pamoja viongozimbalimbali wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay, na Kaimu MkurugenziMtendaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile.
No comments:
Post a Comment