Mkurugenzi Mtendaji wa I&M Group PLC, Bw. Sarit Raja-Shah akikata utepe kuashiria uzinduzi ofisi ya makao makuu yake mapya jijini Dar es Salaam katika Barabara ya Haile Selassie, Masaki.
Picha ya pamoja.
BENKI ya I&M Tanzania katika kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake nchini Kenya. Imezindua ofisi ya makao makuu yake mapya jijini Dar es Salaam katika Barabara ya Haile Selassie, Masaki.
Katika kumbukizi hiyo iliambatana na hafla fupi iliyowaleta pamoja watu mbalimbali ikiwemo wateja wa Benki hiyo na kuangazia chimbuko la benki hiyo, ilipotoka, inakoelekea na ukuaji wake wa kasi.
Hafla hiyo ilifanyika katika makao makuu mapya ya Benki ya I&M Tanzania jijini Dar es Salaam na iliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa I&M Group PLC, Bw. Sarit Raja-Shah.
Katika kuashiria hatua hiyo mhimu katika upanuzi unaoendelea wa benki inayotoa huduma za kipekee za kibenki. Ofisi hiyo mpya, iliyo na vifaa vya kisasa imeanzishwa ili kutoa huduma za kibenki za kisasa zinazozingatia wateja.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa I&M Bank Tanzania, Zahid Mustapha alisema kuwa uzinduzi huo kwa kiasi kikubwa utaongeza uwezo wa benki kuhudumia wateja wake kwa ufanisi mkubwa.
Pia aliwashukuru wateja, wadau, na wafanyakazi wa benki hiyo kwa usaidizi wao katika kufanikisha safari ya benki hiyo.
“Maadhimisho haya ni uthibitisho wa ukuaji wa Benki katika kipindi cha miaka 50 iliyopita na hii ni ishara ya mchango wa Benki ya I&M Tanzania katika uchumi na watu wa Tanzania. Ofisi yetu hii mpya haiwakilishi tu ukuaji wa benki yetu lakini pia ni dhamira yetu inayoendelea ya kutoa huduma zenye ubora na ufanisi. Tunafurahia fursa zinazoletwa na ukuaji wa Taasisi za Kibenki na tunatarajia kuendelea na safari yetu ya ukuaji, iliyojaa mafanikio na inayochagiza kuongezeka kwa wadau na wateja wetu wanaothamini kazi zinazofanywa na benki yetu.” alisema Bw. Zahid.
Kwa Upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya I&M Tanzania wakati akizungumza kwenye hafla hiyo alisema “Benki ya I&M Tanzania imejidhatiti kutoa huduma za kisasa na zenye ubora wa hali ya juu kwa wateja wetu huku ikichagiza ukuaji wa maisha ya watu katika jamii tunazohudumia katika nchi hii kubwa ya Tanzania. Kama Bodi ya Wakurugenzi, tunatoa mwongozo na uangalizi wetu wa karibu kulingana na maadili ya Taasisi yetu na kuendelea kuhamasisha utoaji wa huduma bora kwa watendaji ili kuongeza thamani ya Benki yetu hususani kwa wateja na wadau wetu. Hatua tulizopiga kama Benki ya I&M Tanzania gzisingewezekana bila uungwaji mkono thabiti katika uidhinishaji wa udhibiti na usimamizi na Benki Kuu ya Tanzania. Kwa Benki Kuu ya Tanzania chini ya uongozi wa Mheshimiwa Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba, tunashukuru sana”.
Benki ya I&M imesherehekea kumbukizi yake ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo mnamo mwaka 1974. Nia ya dhati ya ujasiriamali ya Mwanzilishi na Mwenyekiti Emeritus ndio iliyochagiza na kuifanya Benki ya I&M kukua kutoka shirika la kukopesha jamii hadi Taasisi inayotoa huduma za kifedha.
Taasisi hii inatoa huduma mbalimbali za kibenki na za kifedha zinazojumuisha Benki ya Biashara na Kitaasisi, Huduma za Kibenki za Kibinafsi na Biashara, Bancassurance, Usimamizi wa Mali na huduma za Ushauri zinazopatikana katika nchi 5 za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Mauritius.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni mbalimbali, wakiwemo watu mashuhuri kutoka Taasisi za kibenki, viongozi wa makampuni, wateja na wadau mbalimbali wa benki hiyo. Maadhimisho hayo yalijumuisha hotuba zilizojaa hadithi za benki hiyo, kutoka kwa viongozi wa benki hiyo, hotuba zao zilielezea safari ya benki hiyo na michango yake katika uchumi wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment