HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 19, 2024

WATAALAM WA MELIVITA YA JESHI LA UKOMBOZI LA WATU WA CHINA KUTOA HUDUMA MUHIMBILI

 

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amepokea wataalam waliokuja na Melivita ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (CPLA) kwa lengo la kushirikiana na  kubadilishana uwezo na wataalam wa hospitali hiyo.

 Prof. Janabi amesema MNH ina idara mbalimbali ambazo wataalam hao watashirikiana na wenzao  ili kuboresha huduma za afya na kuongeza ujuzi wa watendaji wake.

 Ujio wa meli hiyo unatokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya China ambao umedumu kwa kipindi kirefu.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad