HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 11, 2024

UTEUZI

 


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Mululi Majula Mahendeka, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua na kumuapisha Bw. Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mombo alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu. Bw. Mombo amechukua nafasi ya Balozi Ali Idi Siwa ambaye amestaafu.

Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad