Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbas amewaomba wananchi
kutembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika Maonesho ya
SABASABA kwa lengo la Kujifunza na kuona jinsi serikali ilivyofanya
jitihada katika uhifadhi.
Ombi hilo amelitoa leo Julai 2,2024
Jijini Dar es Salaam alipotembelea Banda la wizara ya maliasili na
Utalii,katika Maonesho ya SABASABA yanayoendelea tangu yalipofunguliwa
Juni 28,2024.
Aidha Dkt.Abbas ametoa hamasa kwa wananchi
kujitokeza ili kujionea wanyama baadhi ambao wamewaweka katika
Maonesho hayo ambapo anaamini watahamasika kwenda hifadhini kujionea
zaidi kwa kile watakacho kiona.
"Banda letu litakuwepo kwa siku
kadhaa zijazo tunawaomba sana wananchi waje hapa Kuna wanyama kama
simba,kuna chui,kuna pundamilia,lakini hapa tumeweka wachache ili
wananchi wapate tamaa ya kwenda kwenye hifadhi zetu,kwenye mapori ya
akiba kujionea kile Mwenyezi Mungu ametubariki Kama taifa"Dkt.Abbas
amesema.
Pamoja na hayo,Dkt.Abbas ameeleza kuwa watakao tembelea
banda hilo watapata fursa ya kupata elimu ya zao la asali pamoja kujifunza namna ya kupanda Miche kwa ajili ya matunda na biashara
"Wakati
naingia kwenye Banda letu sehemu kubwa swali langu lilikua wananchi
wanauliza nini hasa,utashangaa kuona maswali mengi ya wananchi Ni
uwekezaji kwenye eneo la asali na nyuki wafanye nini,wachukue hatua gani
kwahiyo hii imetupa picha frani watu wengi wanataka kuhamasika katika
biashara ya kufuga nyuki na kuzalisha asali"Dkt.Abbas ameeleza.
Vilevile,Dkt.Abbas
amepongeza jitihada za serikali katika sekta ya Utalii ambapo
imechangia kuongezeka kwa idadi ya Utalii wa ndani ambao ni zaidi ya
Millioni 1.5 wakati huohuo ongezeko la watalii wa nje ambao ni million
1.8.
Tuesday, July 2, 2024
Home
Unlabelled
WANANCHI WATEMBELEA BANDA LA MALIASILI NA UTALII KUJIFUNZA UHIFADHI
WANANCHI WATEMBELEA BANDA LA MALIASILI NA UTALII KUJIFUNZA UHIFADHI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment