HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 6, 2024

NBAA yawahimiza Vijana kuchangamkia fursa za uhasibu


BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imewahimiza vijana wa kitanzania nchini kuchangamkia fursa za uhasibu na ukaguzi kutokana na kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo endelevu ya Taasisi, makampuni ili kuleta tija kwenye ukuaji wa uchumi na ujenzi wa Taifa.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu, Julai 6, 2024 Jijini Dar es Salaam katika maonyesho ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.

"Tunasimamia vigezo vya uandaji wa hesabu za kimataifa na kuhakikisha wanachama wetu wanazingatia maadili na vile vigezo ambavyo vinafanya tasnia ya uhasibu iwe na heshima na mchango unaotarajiwa na wananchi" amesema CPA Prof. Sylvia Temu

Prof. Sylvia Temu ameongezea kuwa ushiriki wao katika maonyesho hayo ni kutoa elimu na kusikiliza sana wadau ili kupata maoni ya mbalimbali na wanatoa mrejesho gani juu ya kazi zinazofanywa na NBAA ili kuboresha zaidi kazi zetu.

Hivyo, Prof. Temu amesema kila kitu kinachofanywa ni lazima kuzingatia viwango ambavyo vinavyosisitiza uendelevu wa huduma, uzalishaji na utunzaji wa mazingira.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa NBAA Magreth Kageya alipotembelea banda la Bodi hiyolililopo katika Jengo la Wizara ya Fedha  katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam. Wa Kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Shirika kutoka NBAA CPA Kulwa Malendeja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Bodi hiyolililopo katika Jengo la Wizara ya Fedha  katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la Bodi hiyo lililopo katika Jengo la Wizara ya Fedha  katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu  akiwa kwenye picha ya pamoja na Wafanyakazi wa NBAA alipotembelea banda la Bodi hiyolililopo katika Jengo la Wizara ya Fedha  katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam. Wa nne kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Shirika kutoka NBAA CPA Kulwa Malendeja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad