HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 2, 2024

Kampuni kuagiza Siagi isiyo na rehemu kutoka Mauritius


Wakala wa kampuni ya WEXCO, Mohamed Barkat akihudumia wananchi waliofika kwenye banda lake kwenye maonyesho ya 77 yanayoendelea jijini Dar es salaam.

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya World Exchange Company Limited (WEXCO), kwa kushirikiana na Quality Beverages ya Mauritius, wanatarajia kuanza kuingiza nchini siagi yenye virutubisho nane na ambayo ni bora kwa afya na mazingira.

Akizungumza leo kwenye maonyesho yanayoendelea kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mauzo ya Nje wa kampuni ya Quality Beverages, Preetam Appadu, alisema bidhaa kutoka nchini humo zinatarajiwa kuanza kuja nchini ndani ya mwezi mmoja.

“Sifa kubwa za siagi hii ni kwamba ina vitamin zaidi ya nane haina rehemu na ni nzuri kwa matumizi kwa watu wenye sukari na presha na imetengenezwa mahsusi kwa matumizi ya watu wenye shida ya sukari na shinikizo la damu,” alisema

“Ina aina nane za vitamin haina rehemu, inaongeza radha ya utamu kwenye chakula nani nzuri zaidi kwenye kuoka mikate, kupikia kukaanga na kupaka kwenye mikate nani bora kwa afya na mazingira,” alisema.

Alisema siagi hiyo imepata mwitikio mkubwa sana maduka mbalimbali yameichangamkia na wameomba wawe wanauza kwasababu baada yaa kuanza kuitumia wameifurahia sana.

“Ndani ya mwezi mmoja tunatarajia siagi ya aina yake kutoka Mauritius itaanza kuingia nchini kwa kushirikiana na kampuni ya WEXCO Tanzania Limited kwa hiyo watanzania watapata bidhaa yenye viwango vya hali ya juu ambayo wataifurahia kwasababu mataifa mengi ambayo tumepeleka bidhaa hii wameipenda,” alisema

Wakala wa WEXCO hapa nchini, Barkat Mohamed alisema kampuni hiyo imekuwa ikisafirisha nje ya nchi bidhaa kama avocado, bilinganya, pasheni, karafuu, tangawizi, vitunguu swaumu, kahawa na cocoa.

“Sisi ni kampuni kubwa yenye uzoefu katika kuagiza na kuuza nje ya nchi bidhaa mbalimbali na ndani ya mwezi mmoja tunatarajia kuanza kuingiza nchini siagi ya kipekee ambayo imetokea kupendwa na watu wengi kwani haina rehemu,” alisema

Alisema itakapoanza kuingizwa nchini itasambazwa kwenye maduka mbalimbali makubwa hivyo aliwataka watanzania kuchangamkia bidhaa hiyo mara tu itakapoingia sokoni kwa mara ya kwanza

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad