HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 11, 2024

FCC YATOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI ZAIDI YA 100 WANAOSIMAMIWA NA SIDO

 

Na Mwandishi Wetu

TUME ya ushindani (FCC) imetoa mafunzo kwa Wajasilamali zaidi ya 100 wanaosimamiwa ba Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO) ikiwa ni muendelezo wa kuwapatia elimu wafanyabiashara ili watambue na kuielewa time hiyo.

Mafunzo hayo yametolewa katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Ofisa Mlinda Mlaji Mkuu (FCC) Magdalena Hall ametumia nafasi hiyo kueleza lengo la Mafunzo hayo ni muendelezo wa elimu ambayo wamekuwa wakiitoa kwa wafanyabiashara kutambua majukumu ya tume hiyo.

"Tumekuwa na mkakati wa kuhakikisha tunatoa mafunzo yanayolenga kuzungumzia shughuli tunazofanya na umuhimu wa FCC.Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wajasiriamali hao maana wao ni wazalishaji wa bidhaa na niwalaji wa mwisho."

Ameongeza ni wajibu wa wajasiriamali hasa wazalishaji kujua wajibu wao na kujisajili ili watambulike FCC maana ni wajibu kulinda nembo zao.

"Tunatoa mwito kwa wajasiriamali hasa wazalishaji kuja Tume ya Ushindani  wajisajili na watambulike ili bidhaa zao zilindwe kisheria na ziwaletee mafanikio", amesema.

Pia amesema ni vyema wajasiriamali kufahamu  mikataba wanayoingia ni lazima isajiliwe na FCC ili kulindwa kisheria.

Kwa upande Christopher Dionis ambaya ni mmoja wa wajasiriamali hao ameishukuru FFC kwa elimu kuwapatia Mafunzo hayo kwani yatachangia kuboresha bidhaa zao ili kukuza uchumi wa nchi. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad