HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 7, 2024

DMI KUSAJILI WANAFUNZI BURE PASIPO MALIPO

Chuo Cha Bahari Dar ES Salaam (DMI) kinaendelea na huduma ya usajili wa wanafunzi katika viwanja vya Sabasaba Dar es Salaam bila malipo.

DMI ni moja ya taasisi zilizopo katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Timu ya wataalam kutoka chuo Cha Bahari Dar es Salaam -DMI wanaendelea kutoa elimu ya masuala ya ubaharia pamoja na fursa zinazopatikana baharini.

Aidha chuo Cha Bahari Dar es Salaam -DMI kinawakaribisha wananchi kutembelea kwenye Banda lao lililopo ndani ya KARUME HALL.

Huduma mbalimbali zinatolewa ikiwa ni pamoja na usajili wa wanafunzi wanaojiunga na Kozi za Cheti na Diploma bila malipo yoyote pamoja na elimu ya Ubaharia.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad