HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 2, 2024

Bodi ya FCC yafanya ziara katika Kituo cha Sirari Ziara yaibua umuhimu wa kuwepo maafisa ukaguzi katika vituo vya mipakani

 

 

Na Mwandishi Wetu,Mara
 
Bodi na Menejimenti ya Tume ya Ushindani (FCC) imetembelea Kituo cha ukaguzi wa pamoja (OSBP) kilichopo Sirari Wilayani Tarime Mkoani Mara.

Kutembelea kituo hicho ni kupata uelewa wa pamoja kuhusu shughuli za ukaguzi mipakani.


Akizungumza katika ziara hiyo ya kutembelea hivi karibuni ,Mkurugenzi Mkuu wa FCC William Erio ambaye pia ndiye Mkaguzi Mkuu wa Alama za Bidhaa Nchini, amebainisha kuwa lengo la ziara hiyo katika Kituo hicho ni kufahamu umuhimu wa kuanzisha ofisi yake
katika eneo hilo na kuongeza jitihada za kutokomeza uingizaji wa bidhaa bandia nchini.

Kwa mujibu wa Erio, uanzishwaji wa Ofisi ya FCC katika kituo hicho utaongeza ufanisi katika ukaguzi na udhibiti wa uingizaji wa bidhaa
bandia na kuongeza Ushindani katika soko la bidhaa nchini.


"Njia zisizo rasmi katika uingizaji wa bidhaa katika mipaka ya nchi yetu ni tatizo kubwa sana katika Ushindani wa biashara nchini na Nchi yetu ni kubwa na mipaka ni mikubwa kwahiyo inatakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa Umma ndio maana tunataka kuanzisha ofisi katika kituo cha pamoja cha ukaguzi," alisema Erio.

Mwenyekiti wa FCC Dkt. Aggrey Mlimuka, baada ya mazungumzo na wasimamizi wa vitengo mbalimbali vya Serikali ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamekiri kuhitaji msaada wa FCC katika kuimarisha uingizaji wa bidhaa kutoka nchi jirani.

"Hakuna sababu wala siyo suala la kujadiliana, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alishatoa maelekezo kuhusiana na suala hilo, hivyo Menejimenti tunaenda kujipanga ili tulete watu wa FCC katika kituo hiki kwa ajili ya kuanza kazi.

"Tupo hapa llkuwatumikia watanzania, Serikali ipate mapato na watu wapate bidhaa ambazo zinastahili kuzwa kwao," alisema Dkt.Mlimuka.

Akizungumza kwa niaba ya Taasisi za Serikali zilizopo katika kituo hicho, Meneja Msaidizi wa Forodha wa TRA Mkoa wa Mara, Said Hemed, aliahidi kutoa nafasi katika kituo hicho ili kuwezesha uanzishwaji wa Ofisi ya FCC huku akisema uanzishwaji wa ofisi hiyo utaongeza tija kwenye ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa uingiaji wa bidhaa zisizo halali.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad