HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 25, 2024

WAZIRI JAFO AOMBA USHIRIKIANO KUKABILI MABADILIKO YA TABIANCHI

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabinchi

Akizungumza leo tarehe 24 Juni, 2024 ofisini kwake jijini Dodoma, Dkt. Jafo amesema changamoto hiyo ya mazingira inamgusa kila mmoja hivyo ni muhimu wadau hao kushiriki kikamilifu katika kukabiliana nayo.

Amewaomba washirika wa maendeleo kupitia taasisi mbalimbali nchini na nje ya nchi kuweka kipaumbele suala la hifadhi ya mazingira kwa kutenga kiasi cha fedha hususan katika zoezi la upandaji wa miti.

Halikadhalika, amewapongeza wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakishiriki katika kampeni mbalimbali za mazingira Srikali inahakikha kil mmoj anashiriki katika kukabiliana na athari hizo kwa kuwaelimusha wannachi

“Wapo watu ambao kiukweli wanaonesha nia ya dhati kabisa na mwamko wa kushiriki katika kampeni za hifadhi mazingira lakini wanakosa rasilimali kwa ajili ya kutekeleza shughuli hizo hivyo ni wajibu wetu kwa ushirikiano na taasisi tuwasaidie ili waweze kuwafikia wananchi,” amesema Dkt. Jafo.

Aidha, Waziri Jafo amesema kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa Tanzania na dunia kwa ujumla, Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya muda mrefu na muda mfupi katika kukabiliana nazo.

Ametaja mikakati hiyo ni pamoja na kuzinduliwa kwa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 ambayo imeweka mikakati ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimazingira katika maeneo mbalimbali nchini.

Vilevile, Waziri Jafo amebainisha kuwa Serikali inaendelea kuchagiza biashara ya kaboni ili wananchi pamoja na wawekezaji kutoka nje ya nchi kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema Serikali iliandaa Kanuni na Mwongozo wa Taifa wa Usimamizi wa Biashara ya Kaboni nchini kwa lengo la kuweka utaratibu na masharti ambayo wadau na wajasiriamali wa biashara ya kaboni watapaswa kuzingatia wakati wa utekelezaji wa miradi mipya na miradi.

Pamoja na hayo, pia Dkt. Jafo amesema katika kuwezesha utoaji wa taarifa za hali za hewa nchini ambazo zinagusa moja kwa moja eneo la mazingira, Serikali imewekeza katika Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Amesema kuwa taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinawasaidia wananchi kujiandaa na hata kujikinga au wasipate madhara makubwa wakati wa matukio ya kimazingira yakiwemo vimbunga au mvua kubwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad