HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 11, 2024

UTEKELEZAJI WA MPANGO JUMUISHI WA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII WAANZA RASMI KATIKA MKOA WA PWANI

 

Mhe Abubakari Kunenge Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

SERIKALI ya Awamu ya Sita (6) inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza rasmi utekelezaji za Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.

Hayo yamesemwa Juni 10,2024 na Mhe Abubakari Kunenge Mkuu wa Mkoa wa Pwani katika Semina Elekezi kwa Viongozi wa mkoa huu na Wilaya zake kuelekea katika utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ulizinduliwa hapo awali (mwezi Januari, 2024) na Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akitoa salamu za ufunguzi, Mhe. Kunenge ameishukuru Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kuupa kipaumbele Mkoa wa Pwani na kuahidi kuwa mkoa huo utakua mkoa wa mfano katika utekelezaji wa Mapngo huu. Vilevile ameelekeza Mamlaka husika na Viongozi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika hatua zote za utekelezaji. Zoezi la kuwachagua Wahudumu hawa katika Mkoa wa Pwani litaanza katika Halmashauri mbili (2) za kibaha Mji na Rufiji ambapo jumla ya Wahudumu 480 watafikiwa.

Akizungumza wakati wa Mkutano huo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mkoa huo amesisitiza kusimamia kikamilifu hatua zote za utekelezaji wa Mpango huu.

Meshack Chinyuli Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya.

Naye mwakilishi wa Wizara ya Afya Dkt. Meshack Chinyuli amesema utekelezaji unaoendelea unalenga kuhakikisha uimarishaji wa huduma za afya ngazi ya jamii ili kuboresha huduma za afya ngazi ya msingi na kufikia dhana ya afya kwa wote ifikapo mwaka 2030.


Imeelezwa kuwa Serikali imedhamiria kufikia jumla ya Wahudumu 137,294 katika Mikoa yote ya Tanzania Bara katika kipindi cha miaka mitano (5).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad