Na Mwandishi Wetu, Mbeya
SHIRIKA
la Viwango Tanzania (TBS), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini limeteketeza
tani 7.2 za bidhaa hafifu zikiwemo zilizoisha muda wake wa matumizi
vikiwemo vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 43.
Miongoni vya
bidhaa zilizoteketezwa ni vipodozi vyenye viambata sumu ambavyo
vimepigwa marufuku kutumika nchini, vinywaji vyenye vilevi vilivyoisha
muda wake wa matumizi (Bia, Mvinyo), juisi, soda, vinywaji vya kuongeza
nguvu (energy drink), mafuta ya kula, biskuti, maziwa ya watoto, tomato
na chili sauce, blue band na bidhaa zingine mbalimbali.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkoani Mbeya leo wakati wa kuteketeza bidhaa
hizo, Meneja wa TBS, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Abel Mwakasonda,
amesema bidhaa hizo zilikamatwa katika kipindi cha Julai, 2023 hadi
Juni, mwaka huu kufuatia ukaguzi uliofanyika katika halmashauri za Mikoa
ya Mbeya, Songwe, Njombe na Iringa.
Alitaja bidhaa za vipodozi
zilizoteketezwa kutokana na kupigwa marufuku katika soko la Tanzania ni
vile venye viambata sumu venye madini kama Zebaki (Mercury), madini
Tembo (Lead) na Hydroquinone.
Alisema bidhaa hafifu
vilivyoteketezwa pamoja na vipodozi pindi vinavyotumiwa na watumiaji
vinasababisha madhara mbalimbali ya kiafya. Miongoni mwa madhara ya
kiafya yanayosababishwa na bidhaa hizo kwa mujibu wa Mwakasonga ni
magonjwa ya matumbo, saratani ambapo vipodozi hivyo vinaondoa asili ya
ngozi pamoja na kusababisha madhara mengine mbalimbali katika mwili wa
binadamu.
Alitoa rai kwa wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa
bidhaa mbalimbali kuhakikisha kuwa wanaingiza sokoni bidhaa ambazo
zimethibitisha ubora wake na TBS, vinginevyo zitaondolewa sokoni na
kuteketezwa kwa gharama zao wenyewe.
Kwa mujibu wa sheria ya
viwango ni marufuku kwa wazalishaji, wazambazaji na wauzaji kuingiza
kwenye soko la Tanzania bidhaa ambazo hazijathibitishwa ubora wake na
TBS.
Mwakasonda, alisema ukaguzi wa bidhaa sokoni unafanywa kwa
kuzingatia Sheria ya Viwango Na:2 ya mwaka 2009 na kanuni zake za mwaka
2021 sambamba na Sheria ya Fedha namba Na: 8 ya mwaka 2019.
Aidha,
Mwakasonda aliwataka wananchi kutotumia bidhaa ambazo hazijathibitishwa
na TBS zikiwemo zile zilizopigwa marufuku kutumika nchini vikiwemo
vipodozi vyenye viambata sumu.
Alisisitiza wananchi kusoma
taarifa zilizopo kwenye vifungashio vya bidhaa wanazotaka kununua ili
kujua kama hazijaisha muda wake wa matumizi na kama zimethibitishwa na
TBS.
Friday, June 21, 2024
Home
Unlabelled
TBS YATEKETEZA TANI 7.2 ZA BIDHAA HAFIFU KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI
TBS YATEKETEZA TANI 7.2 ZA BIDHAA HAFIFU KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment