HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 26, 2024

NEEC YASHAURI MAKUNDI YA KINAMAMA YAJIANDAE KUFANYA BIASHARA NA VIWANDA NA MIRADI YA SERIKALI


Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng'i Issa akizungumza na Makundi ya Kinamama, Vijana na Makundi Maalumu wakati Baraza hilo lilipoifikisha program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Patrick Sawala kushoto ni Mtaalamu katika timu ya IMASA, katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Dar es Salaam Dr.Elizabeth Mshote
Matibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa akizungungumza na Makundi ya Kinamama, Vijana na Makundi Maalumu hawapo pichani wakati baraza hilo lilipoifikisha program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Patrick Sawala.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng'i Issa akizungumza na Makundi ya Kinamama, Vijana na Makundi Maalumu hawapo pichani wakati baraza hilo lilipoifikisha program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Patrick Sawala.
Makundi ya Kinamama, Vijana na Makundi Maalumu wa Mkoa Mtwara wakipata mafunzo ya ujasiriamali wakati Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lilipoifikisha program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) mkoani Mtwara.
Picha na mwandishi wetu

Na Mwandishi Wetu
BARAZA la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kupitia program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) limeshauri makundi ya kinamama, vijana na makundi maalumu Mkoaani Mtwara kujisajili kupata sifa ya kufanya biashara na viwanda vikubwa na miradi mbalimbali ya serikali ili kuondokana na hali duni ya vipato na kushiriki katika uchumi wa taifa.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng'i Issa alitoa ushuri huo kwa makundi hayo jana wakati Baraza hilo lilipoifikisha program ya IMASA katika Mkoa wa Mtwara kuwa makundi hayo yanahitajika kujisajili na kukidhi vigezo ili yaweze kuunganishwa kufanya biashara na viwanda vikubwa na miradi mbalimbali ya serikali kwa nia ya kuondokana na vipato duni na kushiriki katika uchumi wa taifa.

“Mkoa huu wa Mtwara unafursa ya uwepo wa viwanda vikubwa na miradi mbalimbali ya serikali inayotekelezwa na inayokuja mtaunganishwa nayo kibiashara ili mshiriki katika uchumi wa taifa, na hii ndiyo kazi ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi, alisema Bi. Beng'i.

Alisema katika Mkoa wa Mtwara kuna miradi inakuja ikiwemo ya gesi, upanuzi wa Uwanja wa Ndege na Bandari hivyo makundi hayo au wafanyabiashara watahitajika kutoa huduma za bidhaa kama za Saruji, Mchanga, Kokoto, na hata Chakula, Ulinzi pamoja na Usafi.

Akifafanua zaidi alisema uwekezaji unaofanywa na wageni au wafanyabiahara wa ndani lazima kuwe na mpango wa kushirikisha watanzania kupata ajira za ujuzi na zisizo za ujuzi na kutoa huduma mbalimbali.

Bi, Beng'i alisema ili kupata fursa hizo wanahitajika kujipanga kuwa katika vikundi hivyo au mtu mmoja moja na kusajiliwa kwa kuwa na vitambulisho vya NIDA, Akaunti za Benki, kuwa na biashara na mitaji na hiyo itasaidia kupata takwimu halisi na kupanga vipaumbele vya Mkoa.

Alisema program hiyo ya IMASA ina awamu mbili ya kwanza kupata taarifa na kutengeneza kanzidata na awamu ya pili ni ya kutoa uwezeshaji na program hiyo ni kwa nchi nzima.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Patrick Sawala alisema wamepokea program ya IMASA na kuitekeleza pamoja na watalaam kuhakikisha wananchi wanatumia fursa hiyo kushiriki katika uchumi wa taiafa lao.

“Tumeleta program nawaomba wananchi mtumie fursa hii kwenye Kilimo, Ufugaji, Uvuvi pamoja na Usindikaji wa mazao , na aliongeza kuwa Mkoa wa Mtwara kuna Kilimo cha Mwani, Ufugaji wa Mjongoo Bahari , Utalii wa Kitamaduni.

Alisema Mkoa wa Mtwara wanatarajia kupata Nishati ya Umeme kwa vijiji vyote na vitongoji vyote ambyo itakuwa chachu ya kuanzisha viwanda vidogo na biashara kusaidia kukuza vipatoa kwa wananchi.

Naye Mwananchi wa katika Mkoa wa Mtwara Bi. Khadija Mela alisema amepata elimu kuwa aliyeanza biashara aendelee na wasionabiashara wajiunge katika vikundi au mtu mmojammoja ili kupata uwezeshaji.

"Watu ambao hawajafika kupata elimu hii wakisikia tena wafike lakini na sisi tunaenda kuwa mabalozi kwa vile ni program inayolenga kutukomboa kiuchumi akinamama,alisema.

Kwa Upande wake Fadhili Ngavuja alisema anashukuru program nia ya kutaka kuwakwamua makundi hayo na yeye amejiunga kwa ajili ya kuingia katika kanzidata ya Baraza ili kupata uwezeshaji na anatarajia atakuwa kijana mpya na kushiriki kukuza uchumi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad