HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 7, 2024

NCHIMBI AWASILI TANGA, KUHITIMISHA MIKOA 5

Matukio mbalimbali katika picha wakati Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi alipowasili na kupokelewa Mkoa wa Tanga, kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa huo, akitokea Mkoa wa Kilimanjaro.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Ndugu Rajab Abdulrahman Abdallah, aliwaongoza wanachama na viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Tanga, kumpokea Balozi Nchimbi katika eneo la Mombo, Wilaya ya Korogwe, ambapo leo anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika Mji wa Korogwe.

Katika ziara hiyo, yenye malengo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025, kukagua na kuhamasisha uhai wa Chama, pamoja na kusikiliza kero za wananchi, Katibu Mkuu Balozi Nchimbi ameambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmshauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa NEC - Oganaizesheni, Ndugu Amos Gabriel Makalla, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo na Ndugu Rabia Hamid Abdalla, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Katika mapokezi hayo yaliyofanyika eneo la Mombo, Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Wilaya ya Korogwe, Ndugu Nurdin Bakari, alitangaza rasmi kukiacha chama chake hicho cha zamani na kujiunga rasmi CCM, mbele ya Balozi Nchimbi.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad