HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 19, 2024

MAHAKAMA YAKUBALI PINGAMIZI LA EQUITY KATIKA KESI YA MIKOPO CHECHEFU

 



*Pingamizi ni baadhi ya vielelezo vilivvotakiwa kujumuishwa nje ya utaratibu wa kesheria
*Ni katika kesi baina yao na CRC inayotetewa na wakili Mwalongo

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SIKU chache baada ya Makakama ya Rufaa Chini ya Jopo la Majaji Watatu Jaji Rehema Mkuye, Jaji Abraham Mwampashe pamoja na Jaji Zainabu Mruke kubatilisha hukumu ya Kampuni ya State Oil iliyokuwa ikitetewa na Wakili Frank Mwalongo dhidi ya Benki ya Equity Tanzania na Kenya kuelekeza kesi hiyo ianze kusikilizwa upya katika Mahakama ya Biashara

Jana Juni 18,2024 Kampuni ya CRC inayotetewa na Wakili Frank Mwalongo imegonga mwamba baada ya Mahakama Kuu Division ya Biashara Mbele ya Jaji Profesa Ubena Agatho kukubali pingamizi lilowekwa na Wakili Mpaya Kamala kupinga kupokea sehemu ya vielelezo vilivyotakiwa kutumika katika kesi hiyo baina ya CRC na Benki ya Equity

Katika kesi hiyo shahidi wa pili upande walalamikaji Elexender Gombanila amewasilisha nyaraka mbalimbali ikiwa ndio ushahidi katika kesi hiyo ya mkopo Chechefu.

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara imeendelea na usikilizwaji wa shauri la biashara Namba 16 la Mwaka 2023 kati ya kampuni ya CONTINENTAL RELIABLE CLEARING (T) LIMITED ambaye ni mdai katika kesi hiyo Dhidi ya EQUITY BANK TANZANIA LIMITED na Equity BANK KENYA LIMITED ambao ni wadaiwa. Kesi hiyo inayohusiana na mkopo chechefu inasikilizwa mbele ya Mheshimiwa Jaji Professa Ubena Agatho wa Mahakama Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara.

Katika kesi hiyo kampuni ya CONTINENTAL RELIABLE CLEARING (T) LIMITED iliyofunguliwa Mwaka 2023 mdai anaiomba mahakama pamoja na mambo mengine kutoa amri dhidi ya wadaiwa ya kuwa wadaiwa ambao ni taasisi za kibenki wamevunja mikataba ya mikopo na kuvunja wajibu wa benki dhidi ya mdai kama mteja. Pili, Mahakama itamke ya kuwa mdai amelipa mikopo yake yote na hadaiwi. Tatu, Mahakama itamke ya kuwa kiasi cha dola za kimarekani zaidi ya milioni kumi (10,139,664.95) ambazo wadaiwa kwa pamoja wamemtaka mdai alipe kama kiasi cha mkopo ambacho hakijalipwa sio halali na hakijawahi kuwepo. Nne, Mahakama itamke ya kuwa mikopo inayodaiwa kutolewa tarehe 29/05/2018, 3/11/2021 na tarehe 19/02/2022 ni batili. Tano, Mahakama itamke ya kuwa mikopo iliyotolewa tarehe 1-02-2019 na tarehe 17-09-2020 haijawahi kutekelezwa na mdaiwa namba mbili ambaye ni Equity Bank Kenya isipokuwa kwa kiasi Fulani ilitekelezwa na mdaiwa namba moja ambaye ni Equity Bank Tanzania. Sita, Mahakama itamke ya kuwa mikataba ya dhamana zote zisizohamishika zilizowekwa kwa wadaiwa kudhamini mikopo na mdai ni batili. Saba, Mahakama itoe tamko ya kuziondoa dhamana hizo kwenye mikopo na kuzikabidhi kwa mdai. Nane, Mahakama itamke ya kuwa tamko la kutaka wadaiwa walipwe fedha za mkopo na mdai ni batili. Tisa, Mahakama itamke ya kuwa Equity Bank Kenya ambaye ni mdaiwa namba mbili hana leseni ya kuendesha shughuli au biashara ya kibenki au biashara yeyote Tanzania na hivyo amefanya biashara kinyume cha sheria tofouti na matakwa ya kanuni na miongozo inayohusiana na biashara za kibenki nchini Tanzania. Kumi, Mahakama itamke ya kwamba mdaiwa namba mbili amabye ni Equity Bank Kenya hajawahi kutoa au kumpatia mkopo mdai. Kumi na moja, fidia, gharama za kesi na nafuu nyinginezo ambazo mahakama itaona sahihi kuzitoa kwa mdai dhidi ya wadaiwa.

Chimbuko la kesi hii inadaiwa kuwa kwa mujibu wa hati ya madai iliyowasilishwa mahakamani hapo, kati ya Mwaka 2013 mpaka 2017 mdai alikuwa ni mteja wa mdaiwa namba moja, Equity Bank Tanzania. Kwa kipindi chote hicho, mdaiwa alipatiwa mikopo mbalimbali ambayo inafikia minane kwa ajili ya kuendesha biashara zake miongoni mwazo ni biashara ya usafirishaji wa mizigo na mafuta kwa kutumia magari. Ilipofika kuanzia mwaka May 2018 ndipo mdaiwa Equity Bank Kenya alipoanza kuingia kwa kushirikiana na mdaiwa namba moja kwa pamoja kumkopesha mdai.

Kiini cha mgogoro haswa ni mikopo inayodaiwa kutolewa na wadaiwa wote wawili Kwenda kwa mdai iliyosainiwa 29/05/2018, 3/11/2021 na 19/01/2022 kati ya mdai na wadaiwa wote wawili ambapo kwa mujibu wa wadaiwa wanadai kuwa mdai hajalipa kiasi cha dola za kimarekani zaidi ya milioni kumi na hivyo kumtaka alipe pesa hivyo kama alivyokopa kulingana na mikataba ya mikopo. Kwa upande wa mdai anapinga madai ya kulipa pesa hizo kwa sababu ya kuwa ingawa wakopeshaji wametajwa wote wawili kwenye mikopo hiyo, lakini mdaiwa hajawahi kuingiziwa fedha zozote na Equity Bank Kenya wala kulipa pesa zozote kwa Equity Bank Kenya. Na kuhusu fedha alizokopeshwa na Equity Bank Tanzania mdai anasema kuwa aliendelea kuzilipa na ulipaji huo ulithibitishwa kila mara na mdaiwa wa kwanza.

Kwa upande wa majibu ya utetezi yaliyowasilishwa mahakamani kwa pamoja na wadaiwa wote wawili, wanapinga hoja au madai yote yaliwasilishwa mahakamani na mdai na kuiomba mahakama iyatupilie mbali kwa kuwa mdaiwa alikopa kihalali kutoka kwa wadaiwa wote wawili na kwa nyakati tofauti kati ya tarehe 27/05/2020, 19/01/2023, 26/01/2023 na 26/02/2023 mdaiwa kupitia mawasiliano kwa njia ya barua pepe na barua nyingine zilizoandikwa Kwenda kwa wadaiwa alithibitisha kutolewa kwa fedha hizo za mikopo na hivyo hawezi kuitaka mahakama kubatilisha mikataba ya mikopo hiyo baada ya kushindwa kuilipa au kurejesha.

Kesi hiyo leo ilipokuja kuendelea na usikilizwaji, upande wa mdai uliendelea kutoa Ushahidi wake kwa shahidi namba mbili upande wa mdai ambaye Elexender Gombanila

la Upande wa mdai uliwakilishwa na Wakili Msomi Frank Mwalongo ambaye alikuwa wakili kiongozi na upande upande wa wadaiwa uliwakilishwa na Wakili Emmanuel Kagali akimuwakilisha Equity Bank Tanzania Ltd na Wakili Mpaya Kamara akimuwakilisha Equity Bank Kenya Ltd.

Baada ya kuapishwa na Mahakama, shahidi namba mbili wa upande wa mdai aliweza kuwasilisha vielelezo vya Ushahidi ambazo ni nakala 8 za miamala ya Equity Bank (Bank Statements) za kati ya 2013 na 2017 pamoja na barua pepe ambazo zilipokelewa na mahakama bila pingamizi lolote kutoka upande wa utetezi.

Tatizo lilianzia pale ambapo shahidi alitaka kuwasilisha nakala za miamala ya kifedha nne (bank statements) za kati ya 2018 hadi 2022 ambapo zilikumbana na mapingamizi ya kisheria kutoka kwa mawakili wa utetezi. Mapingamizi hayo yalitolewa kupinga kupokelewa kwa nakala hizo za miamala ya kibenki ni kuwa Kiapo cha uthibitisho wa usahihi wa nakala hizo kuwa zimetoka Equity Banks zipo kinyume na sheria ya Ushahidi Sura ya 6 hasa kifungu namba 76, 77 na 78. Vilevile shahidi huyo sio afisa wa benki au Partner wa benki hivyo hana uhalali wa kuzitoa nyaraka hizo.

Pingamizi lingine ni kuwa nyaraka hizo hazijawahi kuwasilishwa au kuongelewa wakati kesi hiyo inafunguliwa kinyume na sheria inayoongoza taratibu za uendeshaji wa kesi za madai (Civil Procedure Code).

Baada ya kutolewa kwa mapingamizi hayo Mahakama iliwapatia nafasi mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja za kisheria ili kuiwezesha mahakama kuamua kama nyaraka hizo zipokelewe kama sehemu ya Ushahidi au zikataliwe mahakama zisipokelewe.

Baada ya mawakili kumaliza hoja zao Mahakama ilipata nafasi ya kuzijadili hoza za mawakili wote juu ya mapingamizi hayo yaliyowasilishwa na upande wa utetezi ili kutoa uamuzi mdogo kuhusiana na mapingamizi hayo.

Mahakama katika uamuzi wake ilikubaliana na mapingamizi yaliyowasilishwa na mawakili wa upande wa utetezi kuwa yanamashiko kisheria na hivyo kukataa kupokea nyaraka hizo. Sababu za kukubaliana na hoja za mawakili wa utetezi juu ya mapingamizi yao ya kisheria ni kuwa kiapo cha shahidi juu ya uthibitisho wa usahihi na uhalali wa taarifa za miamala (bank statements) kinakinzana na matakwa ya kifungu cha 76,77 na 78 ya sheria ya Ushahidi (Evidence Act) Sura 6) kwa kuwa nyaraka hizo hazina sahihi wala muhuri wa benki kwa uthibitisho kuwa zimetoka benki.

Pia shahidi huyo sio afisa au partner wa benki kwa kuwa hakuna sehemu yeyote amethibitisha au kusema kuwa anatokea benki kinyume na sheria ya Ushahidi. Na mwisho, nyaraka hizo hazikuwa sehemu ya nyaraka zilizowasilishwa mahakamani wakati wa kufunguliwa kwa kesi hiyo kinyume na matakwa ya sheria za mwenendo wa mashauri ya madai.

Baada ya kusoma uamuzi huo mdogo na kukataliwa kupokelewa kwa nyaraka hizo, shahidi aliendelea kutoa Ushahidi wake hapo mahakamani.

Wakati shahidi anaendelea kutoa Ushahidi wake hapo mahakamani, kulitokea pingamizi linguine lililotolewa na mawakili wa upande wa utetezi kuomba mahakama kukataa kupokea nyaraka nyingine iliyotolewa na shahidi kuonesha malipo mbalimbali ambayo ni kinyume na sheria kwa kuwa shahidi huyo sio mtu sahihi kuwasilisha nyaraka hiyo, nyaraka hiyo haijawahi kutolewa awali wakati wa kufungua kesi mahakamani na hakuna kiapo kuthibitisha usahihi wa nyaraka hiyo (affidavit of authenticity) ya shahidi huyo.

Baada ya kuwapa nafasi mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja zao juu ya mapingamizi hayo, shauri lilihairishwa mpaka kesho saa nne (Leo) asubuhi kwa ajili ya kutolewa uamuzi mdogo kama nyaraka hiyo ipokelewe au isipokelewe na mahakama kama sehemu ya Ushahidi wa mdai.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad