Mazungumzo yao yalihusu ushirikiano katika kufikia #AfyaKwaWote na kupunguza vifo vya watoto wachanga barani Afrika na duniani kote.
Katika mazungumzo hayo, Bi. Mollel alielezea jinsi ambavyo Taasisi ya Doris Mollel inafanya kazi nchini Tanzania, hasa katika kuboresha miundombinu ya utoaji huduma kwa watoto wachanga, hasa wale wanaozaliwa kabla ya wakati.
Kwa upande wake, Dr. Tedros aliipongeza Taasisi hiyo kwa juhudi zake katika mapambano hayo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano.




No comments:
Post a Comment