HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 18, 2024

BRELA KUANZA KUTOA TUZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZA BIASHARA

Na Said Mwishehe,Michuzi TV - Morogoro 

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA) wataanza kutoa tuzo Maalum kwa waandishi wa habari za biashara ambao watakuwa wakiandika makala zenye matokeo chanya kwa jamii lakini makala ambazo zitakuwa zimejitosheleza.
 
Ameyasema hayo leo Juni 18, 2024 jijini Morogoro,Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA (BRELA) Godfrey Nyaisa wakati wa Mafunzo Maalumu ya BRELA kwa Waandishi wa habari wanaoripoti Mkoa wa Dar es Salaam ambapo lengo ni kuwajengea uwezo utakaowezesha waandishi hao kuandika kwa weledi habari za Wakala huo.
 
"Tutakuwa na tuzo maalum kwa waandishi wa habari ambao watakuwa wanaandika Makala zinazohu BRELA.Tutakuwa tunashindanisha makala hizo na mshindi wa kwanza ambaye atakuwa ameandika makala Bora atapewa tuzo na itakuwa ENDELEVU,"amesema Nyaisa katika mafunzo hayo ambayo ni ya kwanza kutolewa na Wakala huo.

Aidha amesema sababu za kuandaa mafunzo hayo ni utekelezaji wa maelekezo ya vikao vya Wakala huo.

Amefafanua kuwa wameanza na waandishi hao wa habari za biashara kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na hasa wanaondika habari za BRELA lakini mikakati yao ni kwamba mafunzo hayo yatatolewa kwa waandishi wa Mikoa yote na lengo ni kuhakikisha wanaendelea kuwajengea uwezo wadau muhimu wakiwemo waandishi wa habari.

"Tumeamua kuandaa mafunzo haya baada ya kuona habari zinazohusu BRELA zina mambo mengi yakiwemo ya kisheria,hivyo ni vema waandishi wa habari tukawajengea uelewa na kuwawezesha kuwa na ufahamu wa kutosha wa kuandika habari zinazohusu taasisi hii .

"Tumeshuhudia baadhi ya habari ambazo zinaripotiwa lakini Zina makosa mengi,lakini tuona kinachohitajika ni elimu  ili kuondoa makosa hayo huku akisisitiza kwamba kupitia Wakurugenzi wa Wakala huo watatoa elimu ya kutosha katika mafunzo hayo na waandishi wa habari wasisite kuuliza kwa lengo la kujifunza zaidi,"amesema Nyaisa.

Aidha amesema mpango wa mkakati wa BRELA ni kuwa na kanzi data ya waandishi wa habari ambao watakuwa wanaandika habari za Wakala huo ili kusaidia kuwa na habari zenye usahihi na kwamba mafunzo hayo yanaendelea kutolewa sambamba na kuwaita katika matukio yanayohusu BRELA.

Kuhusu majukumu ya BRELA ni  pamoja na kusajili Makampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, Viwanda vidogo, kutoa Hataza, Leseni za Biashara kundi A na Leseni za Viwanda. Menejimenti na Wafanyakazi wa BRELA, wapo tayari kukusikiliza na kutoa huduma bora ili kufanikisha lengo lako.
,Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA (BRELA) Godfrey Nyaisa akizungumza wakati wa Mafunzo ya BRELA kwa Waandishi wa Habari wanaoripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akifungua Mafunzo ya Siku Nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari ambao wanaripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akifungua Mafunzo ya Siku Nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari ambao wanaripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akifungua Mafunzo ya Siku Nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari ambao wanaripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Mwandishi wa habari wa Radio Uhuru, Elias Julius akizungumza jambo wakati wa Mafunzo ya Siku Nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari ambao wanaripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Mwandishi wa habari wa TV E, Hellen Manyangu akizungumza jambo wakati wa Mafunzo ya Siku Nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari ambao wanaripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na viongozi wengine wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari wa magazeti wakati wa Mafunzo ya Siku Nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari ambao wanaripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na viongozi wengine wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari wa Redio wakati wa Mafunzo ya Siku Nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari ambao wanaripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.



Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo ya Siku Nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari ambao wanaripoti Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika mkoani Morogoro.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad