HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 16, 2024

TADB, EXIM KUTOA BILIONI 30 ILI KUWAWEZESHA MITAJI WAKULIMA


Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Frank Nyabundege (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa fedha wa benki ya Exim, Shani Kinswaga wakionesha mikataba mara  baada ya kusaini makubaliano ya kutoa mkopo wa Sh. Bilioni 30 kwa wakulima, wafugaji na wavuvi kwa kipindi cha miaka mitano. 

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Frank Nyabundege (kushoto) akipeana mkono na Afisa Mtendaji Mkuu wa fedha wa benki ya Exim, Shani Kinswaga mara  baada ya kusaini makubaliano ya kutoa mkopo wa Sh. Bilioni 30 kwa wakulima, wafugaji na wavuvi kwa kipindi cha miaka mitano.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Frank Nyabundege (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa fedha wa benki ya Exim, Shani Kinswaga (kulia walioketi) wakisaini mkataba wa makubaliano ya kutoa mkopo wa Sh. Bilioni 30 kwa wakulima, wafugaji na wavuvi kwa kipindi cha miaka mitano. Wanashuhudia nyuma yao kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria TADB Dkt. Edson Rwechungura na kulia Ni Mwanasheria Mkuu Benki ya Exim Edmund Mwasaga
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Frank Nyabundege akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  leo Mei 16, 2024 juu wa ushirikiano baina ya TADB na Exim Benki kuwapatia mkopo nafuu wakulima wadogo. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa fedha wa benki ya Exim, Shani Kinswaga
Afisa Mtendaji Mkuu wa fedha wa benki ya Exim, Shani Kinswaga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  leo Mei 16, 2024 juu wa ushirikiano baina jya TADB na Exim Benki kuwapatia mkopo nafuu wakulima wadogo. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Frank Nyabundege
Picha ya Pamoja.

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo TADB kupitia mfuko wa dhamana wa wakulima imesaini makubaliano na Benki ya Exim ya kutoa dhamana ya mikopo ya jumla ya Sh. Bilioni 30, kwa wakulima, wafugaji, na wavuvi kwa kipindi cha miaka mitano.

Mkataba huo umesainiwa leo Mei 16, 2024 katika makao Makuu ya TADB jijini Dar es Salaam ambapo TADB watachagiza upatikanaji wa mitaji kwa wakulima, kupitia benki ya Exm ambapo watatoa mikopo kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo, mifugo na Uvuvi.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji wa saini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB Frank Nyabundege amesema mkataba huo utasaidia benki ya Exim kuongeza wigo wa utoaji mikopo katika sekta za kilimo,.mifugo na uvuvi hasa kwa wanawake na vijana.

Amesema kuwa fursa hiyo itaziimarisha sekta zote zinazohusu kilimo pamoja na wadau wake kwani ni kwa muda mrefu wakulima nchini walikuwa wakipata changamoto ya mitaji na wengine wakilazimika kukopa kwa masharti magumu na riba kubwa .

Amesema kuwa TADB inatambua changamoto ya mitaji na upatikanaji wa mikopo nafuu inayowakabili wakulima nchini na ndio maana wameongeza nguvu na ushirikiano na mabenki na taasisi na fedha ili kutoa mikopo kwenye sekta za kilimo , mifugo na uvuvi.

Ameongeza kuwa ili kuongeza wigo kwa mabenki na taasisi za kifedha kutoa mikopo zaidi, TADB imefanya maboresho na imeongeza kiwango cha dhamana na kutoa asilimia 50 mpaka 70 kwa miradi ya wanawake, vijana na miradi inayosaidia kupunguza au kukabiliana na athari za mabadiliko yaa tabia nchi jambo litakaloongeza ajira nchini.

"Watu waliokuwa kwenye sekta ya Kilimo wamekuwa wakikosa dhamana, kwa mfano kijana amemaliza chuo leo hana uwezo wa kujidhamini au kule vijijini wanawake ndio wengi kwenye kilimo na ufugaji lakini wanakosa uwezo wa kujidhamini kwa lengo la kukopa sasa sisi TADB tutawadhamini"amesema Nyabundege.

Aidha Nyabundege ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha TADB kutimiza majukumu yake na kutoa wito wa ushirikiano kwa benki na taasisi za kifedha kupitia mfuko wa dhamana wa wakulima wadogo.

"Rais ametuongeza mtaji na fedha zaidi ili kuwafikia watanzania wengi waliokosa dhamana hivyo niwahamasishe Watanzanie wakokope kwa dhamana ya benki TADB tumetanga kiasi cha shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kukopesha na zikiisha tutaongeza nyingine" amesema.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim, Shani Kinswaga amesema ushirikiano huo utakuuza uchumi wa wakulima na taifa kwa ujumla na kuchagiza maendeleo ya kilimo Tanzania.

"Tunaamini ushirikiano huu utakuwa na tija kiuchumi, kimaendeleo kwa wajasiriamali wadogowadogo , vijana , wanawake , makundi mbalimbali ya wafanyabiashara wale wakati na wakubwa ambao wamekuwa wakikosa fursa za kifedha kutokana na masharti ya kukosa dhamana ijapokuwa vigezo na masharti mengine wanakuwa wanaweza kuitimiza" amesema Kinswaga.

Tunashukuru tumeweza kufikia makubaliano na TADB, sisi nia yetu hasa ni kuongeza nguvu na kuhakikisha huduma hizi za mikopo zinawafikia wakulima wengi zaidi nchini na kuwawezesha kufanya kilimo cha kibiashara ili kujikwamua kiuchumi baina yao na nchi kwa ujumla

Amesema Kuwa mikopo hiyo itainua ustawi wa wakilima wadogo wadogo na kilimo chao kitakuwa chenye tija zaidi "mikopo hii yenye masharti nafuu itawasaidia Watanzania kuweza kupata mitaji itakayowawezesha kupiga hatua kutoka kwenye kilimo cha kujikimu na kwenda kwenye kilimo cha Biashara."

Kinswaga pia ametoa wito kwa wakulima, wafugaji, wavuvi, wanawake na vijana kutumia fursa hiyo kuimarisha uchumi wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad